MOURINHO ATAMBA KUPINDUA KIPIGO CHA 3-1 NA KUTINGA NUSU FAINALI UEFA
Eto'o (kulia) akizungumza na Fernando Torres pamoja na Ramires katika uwanja wa mazoezi wa Chelsea wa Cobham
Jose Mourinho akiwa mazoezini na wachezaji wake jana
Jose Mourinho amewata wachezaji wake kuwa na imani ya kuitupa nje Paris Saint-Germain katika mchezo wao wa marudiano wa robo fainali usiku.
Mourinho amesisitiza kuwa kikosi chake kinaweza kupindua matokeo ya kufungwa mabao 3-1 katika mchezo wa kwanza, hivyo mashabiki wawe na imani kwa wachezaji wao katika kipute hicho kitakachopigwa uwanja wa Stamford Bridge
"Kama Paris watatolewa itawauma sana. Kama tutatolewa ndio kitu ambacho watu wengi wanatarajia"
"Nadhani baada ya mechi zote mbili tutakuwa na mabao mengi kuliko wao. Kama sina imani hiyo, sina sababu ya kwenda kwenye mechi na ninafuraha ya kwenda". Alisema Mourinho.
- Naye Kocha wa PSG, Laurent Blanc amesema hawaogopi kukabiliana na Chelsea Stamford Bridge, hivyo mashabiki wao wajiandae kupokea matokeo mazuri.
- Ana matumaini: Kocha wa Paris Saint-Germain Laurent Blanc amesisitiza kuwa timu yake haitayumbishwa na ChelseaMaandalizi: Wachezaji wa PSG wakipasha katika dimba la Stamford Bridge leoNA mtandao
0 comments:
Post a Comment