Wednesday, 9 April 2014

MWEZI MMOJA TANGU NDEGE YA MALAYSIA KUPOTEA DALILI MPYA ZAONEKANA

Kisanduku cheusi cha sauti cha ndege ya MH370 ya Malaysia Airlines iliyopotea kwa zaidi ya majuma matatu, kimeshukiwa kuwa chini ya maji, kwa sasa zoezi la kuitafuta ndege hio limehamia chini ya maji baada ya meli moja ya Uchina inayoshiriki kwenye zoezi hilo kubaini ishara ya sauti ambayo huenda ikawa imetoka kwenye kisanduku cheusi cha ndege hiyo.
Kufuatia taarifa hizo, tayari uchunguzi umeanza kuhusu eneo ambako sauti hizo zilibainika ingawa ni sehemu tofauti kabisa na ile ya awali ambayo ilionekana kwenye picha za Sattelite za nchi ya Australia na China.

Kitengo maalumu kinachoratibu zoezi la utafutaji wa mabaki ya ndege hiyo, kimesema kuwa licha ya dalili nzuri za kubaini sauti hizi, bado hawajapata uhakika wa asilimia mia moja iwapo kile kilichogundulika huenda kikawa ni kisanduku cheusi cha mawasilaino ya ndege hiyo.
Mkuu wa operesheni za Australia kwenye utafutaji wa ndege hiyo, Angus Houston, amesema taarifa hizi zilizotolewa sasa zinaendelea kuchunguzwa kwa umakini mkubwa.
Iwapo kisanduku hicho cha sauti hakitapatikana ndani ya siku mbili zijazo huenda ikawa ngumu zaidi kukipata kwa siku zijazo kwa kuwa siku 30 zimetimia kwa kisanduku hicho kupoteza nguvu yake.
na mtandao

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA