Monday, 7 April 2014

WACHINA WAONA DALILI ZA NDEGE ILIYOPOTEA YA MALAYSIA...

Meli ya China inayofanya kazi ya kutafuta ndege ya Shirika la Ndege la Malaysia iliyopotea maeneo ya Kusini mwa Bahari ya Hindi imepata ishara inayodaiwa kutoka kwenye ndege hiyo, vimesema vyombo vya habari vya China.Vilisema ishara hiyo ilikuwa na marudio ya frikwensi ya 37.5kHz kwa sekunde ambayo ni sawa na ile iliyozalishwa na kinasa sauti cha ndege.
Hata hivyo hakuna ushahidi hadi sasa kama inahusika moja kwa moja na ndege hiyo H370.
Dazeni ya meli na ndege zimeungana kutafuta ndege hiyo, huku operesheni hiyo ikiwa katika kuingia kwa kina katika awamu nyingine ya kutafuta kabla ya betri ya kurekodi data kufifia.
na matukio blg

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA