Alazwa hospitali kwa miaka 45 FULL STORI HII HAPA
Lanjui aliyelazwa katika Wodi Namba Nne katika hospitali hiyo tangu Januari Mosi, 1971, awali alilazwa katika Hospitali ya Sekou Toure, Mwanza kuanzia mwaka 1969 mara baada ya kupata ajali.PICHA|MAKTABA
Lanjui aliyelazwa katika Wodi Namba Nne katika hospitali hiyo tangu Januari Mosi, 1971, awali alilazwa katika Hospitali ya Sekou Toure, Mwanza kuanzia mwaka 1969 mara baada ya kupata ajali.
Singida.
Usiombe yakupate. Abdi Lanjui (75), ametimiza mwaka wa 45 akiwa wodini
katika Hospitali ya Mkoa wa Singida alikolazwa tangu mwaka 1971 baada ya
kupata ajali ya lori.
Lanjui
aliyekuwa dereva wa taasisi aliyoiita "Mamlaka ya Pamba," alipata ajali
hiyo mkoani Mwanza baada ya lori alilokuwa akiendesha kuchomoka gurudumu
la mbele na kupinduka.
"Sababu
ya mimi kugeuza wodi kuwa makazi yangu ya kudumu ni ajali iliyosababisha
kupooza kuanzia kiunoni hadi kwenye nyayo. Kwa kuwa sinyanyuki
kitandani, nimepata vidonda kuanzia makalioni hadi miguuni. Kwa sasa
naishi maisha magumu mno," alisema.
Aomba msaada
Kutokana
na hali hiyo, ameiomba Serikali na jamii kwa jumla kumsaidia chakula kwa
kuwa hana ndugu wa kumsaidia. Lanjui ambaye hawezi kunyanyuka
kitandani, alisema kwa miaka mingi uongozi wa hospitali ya mkoa ulikuwa
ukimhudumia kwa kumpa chakula lakini baadaye huduma hiyo ilisitishwa,
hivyo kumfanya awe ombaomba na maisha yake kuwa ya mlo mmoja kwa siku.
"Kwa vile
siwezi kunyanyuka kitandani na sina ndugu yeyote, nimekuwa nikiwaomba
msaada manesi na watumishi wengine wa hapa hospitali. Nashukuru sana
wamekuwa wakinisaidia bila kuchoka na kuniwezesha kupata walau mlo wa
siku moja," alisema. Lanjui ambaye anazungumza vizuri pia aliomba msaada
wa fedha za kwenda Hospitali ya KCMC, Moshi ili apatiwe huduma zaidi ya
matibabu.
Mwanza hadi Singida
Lanjui
aliyelazwa katika Wodi Namba Nne katika hospitali hiyo tangu Januari
Mosi, 1971, awali alilazwa katika Hospitali ya Sekou Toure, Mwanza
kuanzia mwaka 1969 mara baada ya kupata ajali.
Alisema
akiwa Sekou Toure mwishoni mwa mwaka 1970, hali yake ilibadilika na kuwa
mbaya ndipo alipomwomba mwajiri wake amrudishe nyumbani katika Kijiji
cha Mhintiri katika Wilaya ya Ikungi mkoani Singida ili 'akasubiri kifo
chake.'
Hata
hivyo, alisema uongozi wa Mamlaka ya Pamba ulikataa kumpeleka kijijini
kwake, badala yake ulimkabidhi katika Hospitali ya Mkoa wa Singida mwaka
1971.
Alisema wakati anapata ajali na kulazwa hospitalini, wazazi na ndugu yake wa pekee, walikuwa wamekwishafariki dunia.
Kaimu
Mganga Mkuu wa hospitali hiyo, Mussa Kamala alisema hivi sasa mgonjwa
huyo anahudumiwa na hospitali kama watu wengine wenye ulemavu ambao
hawatozwi gharama yoyote.
Alisema
uongozi wa hospitali uliwahi kumkabidhi kwa Idara ya Ustawi wa Jamii ili
ifanye mipango ya kumrudisha nyumbani, lakini haikuwezekana. Ofisa
Ustawi wa Jamii Mkoa wa Singida, Zuhura Kalya alisema walishindwa
kumrejesha kwao kwani walipofuatilia ilibainika kuwa hana ndugu na
hakukuwa na mtu anayemfahamu kwa sababu aliondoka kijijini hapo mwaka
mmoja baada ya uhuru. CHANZO: MWANANCHI (FS)
via mjengwa
0 comments:
Post a Comment