MFAHAMU HELEN COSTA: KOCHA WA KWANZA MWANAMKE KUFUNDISHA KLABU YA WANAUME ULAYA
Aliyekuwa
kocha wa timu ya taifa ya wanawake ya Irani na Qatar, Helena Costa
ametengeneza historia mpya kwenye soka nchini barani ulaya.
Klabu
ya ligi daraja la kwanza ya Ufaransa Clermont imeweka historia mpya
kwenye soka la nchi hiyo kwa kumtangaza mwanamama Helena Costa kuwa
kocha wao mpya kuanzia msimu ujao, na kumfanya kuwa mwanamke wa kwanza
kufundisha soka la hadhi ya juu nchini Ufaransa.
Costa,
36, alikuwa kocha wa timu ya taifa ya wanawake ya Irani tangu mwaka
2012 lakini sasa amekubali kumrithi Regis Brouard kwenye klabu ya
Clermont.
Helena
ambaye ni raia wa Ureno, aliwahi kufanya kazi kama kocha mkuu wa kituo
cha soka cha klabu ya Benfica na timu kadhaa nyingine nchini Ureno,
ambapo aliweza kushinda makombe kadhaa. Pia aliwahi kuifundisha timu ya
wanawake ya taifa ya Qatar.
NA MATUKIO BLG
0 comments:
Post a Comment