ANGALIA PICHA MWANAMKE AZALIA KWENYE NDOO
Hadija Mohammed, anayetuhumia kukitupa kichanga baada ya kuzaliwa.
MWANAMKE aliyejulikana kwa jina la Hadija Mohammed, mkazi wa Mchikichini, Ilala jijini Dar es Salaam amekumbana na mkono wa sheria baada ya kufanya kitendo cha kinyama kufuatia kujifungulia kwenye ndoo kisha kichanga kukitupa chooni.
Kwa
mujibu wa chanzo, mwanamke huyo alikuwa na ujauzito uliotimiza miezi
tisa na kila mtu alikuwa akiuona, lakini ghafla siku ya tukio baadhi ya
ndugu waligundua kuwa hakuwa na ujauzito tena!
NDUGU WAMBANA
Chanzo hicho
kiliendelea kutiririka kuwa baadhi ya ndugu na majirani walipomuona bila
ujauzito walimbana kwa kumuuliza iliko mimba hiyo.
“Ndugu
zake na majirani walipomuona hana tumbo kama mwanzo walishangaa,
wakaamua kumbana tena kwa vitisho kwamba watampeleka polisi.
“Ndipo alipoamua kueleza ukweli kwamba, alijifungulia kwenye ndoo lakini mtoto alikwenda kumtupa chooni,” kilisema chanzo hicho.
POLISI WAAMBIWA, WAKOMAA NAYE
Habari
zilizidi kudai kuwa baada ya majirani na ndugu kuambiwa hivyo walikwenda
kutoa taarifa kwenye Kituo cha Polisi Pangani kilichopo Ilala, Dar
ambapo walifika na kukiokoa kichanga hicho lakini walikuta kimeshakata
roho.
MAMA APELEKWA POLISI
Mpashaji wetu
alizidi kudai kuwa, baada ya polisi kuuchukua mwili wa mtoto huyo
hawakumwacha mama mtu aendelee kuponda maisha uraiani, walimbeba mpaka
kituoni hapo na kumfungulia jalada lenye namba ILA/RB/1715/2014 kisha
kumpeleka kwenye Mahabusu ya Polisi Msimbazi huku mwili wa mtoto huyo
ukipelekwa Hospitali ya Amana na baadaye Hospitali ya Taifa Muhimbili.
NI FUNDISHO
Afande mmoja
ambaye aliomba jina lake lisiandikwe, alisema ni lazima Hadija apambane
na mkono wa sheria ili iwe fundisho kwa wanawake wengine wenye mchezo
huo.
“Hii
tabia imekua sana. Wanawake wengi wanajifungua kisha wanawatupa watoto
chooni au kokote kusikojulikana ili wao waendelee kula raha mjini. Huyu
lazima sheria ishike makali yake ili iwe fundisho,” alisema afande
huyo.
0 comments:
Post a Comment