CECAFA NILE BASIN CUP: THEM FELIX `MNYAMA` ATIKISA NYAVU MBEYA CITY FC IKIIBAMIZA 3-2 ACADEMIE TCHITE YA BURUNDI
Na Baraka Mpenja
UNAKUMBUKA ule moto wa Mbeya City katika michuano ya ligi kuu soka Tanzania bara msimu uliopita?.
Wawakilishi
hao wa Tanzania wamehamishia kasi yao katika michuano mipya ya CECAFA
Nile Basin Cup, ambapo wameanza vyema mashindano hayo baada ya kuibuka
na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Academie Tchite ya Burundi.
Mabao
ya Mbeya City yamefungwa na washambuliaji hatari Paul Nonga katika
dakika ya 15, Mwegane Yeya dakika ya 27 na nyota mpya Them Felix katika
dakika ya 37.
Mechi
hiyo muhimu kwa Mbeya City fc iliyosuasua kuwasili Sudan kutokana na
kucheleweshewa tiketi za ndege imepigwa katika uwanja wa Khartoum-Sudan.
Kikosi
cha Mbeya City kilichoanza leo ni Barhan David, Kabanda John, Kibopile
Hamad, Julius Deogratius, Yohana Morris, Antony Matogolo, Deus Kaseke,
Mazanda Steven, Paul Nonga, Mwegane Yeya na Them Felix `Mnyama`.
Mbali na mchezo wa Mbeya City fc, majira ya saa 2:00 usiku AFC Leopard ya Kenya itakabiliana na Enticelles ya Rwanda.
0 comments:
Post a Comment