Chris Brown aongezwa muda jela
Brown alifungwa jela baada ya kumchapa aliyekuwa mpenzi wake Rihana
Mwanamuziki wa Marekani Chris
Brown atasalia jela kwa siku nyingine 131 baada ya kukiri kukiuka amri
ya mahakama kuhusu kifungo cha nje alichokuwa amepewa na mahakama.
Muimbaji huyo wa muziki wa mtindo wa R&B
alikiri mahakamani mjini Los Angeles mnamo siku ya Ijumaa kuwa alitenda
uhalifu mjini Washington Oktoba mwaka jana.Brown amekuwa chini ya aungalizi wa mahakama tangu mwaka 2009 alipokiri kumpiga mwanamuziki mwenza na ambaye alikuwa mpenzi wake wakati huo,Rihanna.
Mshindi huyo wa tuzo la Grammy amekuwa kizuizini tangu mwezi Machi alipokamatwa kwa kukiuka amri ya mahakama iliyomweka ndani ya kituo cha ushauri nasaha pamoja na jela.
Kifungo alichopata kuongezewa siku kinahusiana na kisa cha ugomvi kilichotokea mjini DC mwaka jana.
Brown anakabiliwa na mashitaka ya kumchapa mwanamume mmoja nje ya hoteli moja mjini Washington
0 comments:
Post a Comment