KAMPENI ZA KUWANIA URAIS SERIKALI YA WANAFUNZI KATIKA CHUO KIKUU CHA KUMBUKUMBU YA STEFANO MOSHI (SMMUCo) ZAZINDULIWA RASMI
![]() | |
Wagombea urais wakiwa katika uzinduzi wa kampeni nyuma yao ni walinzi wao |
MOSHI. Na KD MULA
Kampeni za kuwania urais katika chuo kikuu cha kumbukumbu ya Stefano Moshi chuo kishiriki cha Tumaini University maarufu SMMUCo zimezinduliwa rasmi hii leo katika campas ya mjini.
Tukio hilo lililo simamiwa na tume ya uchaguzi inayoongozwa na bwana Charles limka(mwanafunzi kozi ya utalii),zilianza kwa kuwakutanisha wagombea wote mbele yawanafunzi walikusanyika katika ukumbi wa chuo hicho ambapo wagombea waliweza kujitambulisha na kujieleza kwa ufupi.
![]() |
bwana Charles Limka akizindua kampeni pembemi ikiwa ni tume ya uchaguzi |
Chuo hiki chenye campus tatu ambazo ni mwika masoka na mjini kilichaonza mwaka 2007 kinashuhudia wagombea wakuu sita katika nafasi ya uraisi pamoja na makamu wakiwa ni Renatus Hemedi urais,toka campus ya mjini akiwa na makamu wake ambaye ni mwanamke pekee katika kinyang’anyiro hiki cha uongozi wa juu Grace Kalinga toka campus ya mwika ,wengine ni Peter Michael nafasi ya urais toka campus ya mwika akiwa na makamu wake Nelson Mushi toka masoka campus na kundi la mwisho ni Billy Francis nafasi ya urais toka campus ya mwika akiwa na makamu wake Pastory Julius .
![]() |
walinzi wa wagombea urais waliokuwa kivutio kikubwa katika uzinduzi huo |
![]() | ||||||||||
Bwana Godwin Tondi mlezi wa wanafunzi campus ya mjini akifuatilia uzinduzi huo |
Akishuhudia tukio hili mlezi wa wanafunzi dosa wa campus ya mjini bwana Godwin Tondi amewaasa wanafunzi kuendesha kampeni za kistaarabu na kudumisha amani ndani na nje ya chuo.
![]() |
wanafunzi wakiwa katika eneo la chuo hicho wakiendelea na shamra shamra |
![]() | |
wanafunzi wakiwa kwenye ukumbi ambapo kampeni hizo zimezinduliwa |
Kampeni hizi zitakazoendeshwa katika campus zote hadi Jumatano ya wiki hii zina lengo la kupata viongozi katika ngazi zote ikiwemo wabunge wa madarasa na makazi wanapoishi wanafunzi wa chuo kikuu cha kumbukumbu ya Stefano Moshi mkoani Kilimanjaro.
0 comments:
Post a Comment