DEREVA AKIMBIA GARI LAKE MCHANA KWEUPE
Na KD MULA
Moshi.
Dereva ambaye jina
lake halikufahamika kwa haraka ametelekeza gari lake baada ya kukimbizwa na
askari polisi jana majira ya saa tano.
Chanzo cha habari kimeeleza kuwa dereva huyo alisimamishwa
na askari wa usalama barabarani ili waweze kulikaguwa gari hilo lakini alikiuka agizo
hilo na kukimbia lakini polisi huyo aliweza kutoa taarifa haraka kwa askari
wenzake na kuanza kumfuata dereve huyo kwa kutumia usafiri wa pikipiki
Walipofika maeneo ya Mbuyuni dereva huyo alishindwa mchaka
mchaka huo na kushuka ndani ya gari akikimbilia pasipojulikana.
Askari polisi hao walisema kuwa gari ya dereva huyo ilikuwa na makosa mengi sababu iliyomfanya
kugoma kusimama pale aliposimamishwa na
askari wa usalama barabarani maarufu kama traffic moja ya kosa alikuwa nalo ni
kutolipa mapato ya TRA
“Baada ya kupata taarifa kutoka kwa askari wa barabani na
kututajia namba ya gari hilo sisi tulianza kulitafuta na kuanza kulifukuzia kwa
nyuma lakini ilipofika maeneo ya mbuyuni dereve huyo aliweza kushuka ndani ya
gari na kulikimbia gari lake” alisema mmoja wa askari waliohusika na operesheni
hIyo (jina kapuni).
CREDIT(PICHA) MOHAMED MGANGA
0 comments:
Post a Comment