Gharama za maisha zapaa Samunge
Maelfu ya vijana kutoka sehemu mbalimbali nchini wapo Samunge kuchimba
dhahabu katika Mto uliokauka wa Karabaline huku wakisema wanapata
dhahabu yenye ubora wa juu kuliko ya mahali pengine.PICHA|MAKTABA
Na Mwandishi Wetu, Mwananchi
Posted Alhamisi,Mei22 2014 saa 24:0 AM
Posted Alhamisi,Mei22 2014 saa 24:0 AM
Kwa ufupi
Ndoo ya maji Sh2,000 sahani ya wali Sh6,000, Babu aomba msaada wa Serikali
Maelfu ya vijana kutoka sehemu mbalimbali nchini
wapo Samunge kuchimba dhahabu katika Mto uliokauka wa Karabaline huku
wakisema wanapata dhahabu yenye ubora wa juu kuliko ya mahali pengine.
Baadhi ya wachimbaji kutoka Mikoa ya Kanda ya
Ziwa, Morogoro na Msumbiji, walisema dhahabu inayopatikana katika mto
huo ambao umevamiwa kwa zaidi ya kilomita nne, inaelezwa imesambaa hadi
katika mashamba na milima ya Kijiji cha Mgogo, Samunge.
Mchimbaji Mashaka Kasunga alisema dhahabu ya hapo haipatikani maeneo mengine nchini.
Alisema yeye na wenzake 30 wenyeji wa Ushirombo,
Shinyanga ndiyo walikuwa wa kwanza kuchimba madini hayo Aprili mwaka huu
baada ya kupata taarifa ya kuwapo kwake.
“Tulikuwa Singida machimboni ikaletwa dhahabu
iliyotolewa mlimani hapa tukaiona ni bora sana ndipo tukaja tukachimba
awamu ya kwanza na kupata gramu 116 na tukaenda kuuza,” alisema.
Mchimbaji John Kefa alisema hajui walipata gramu
kiasi gani lakini wachimbaji wengine walipata kilo moja ya dhahabu
ambayo waliuza zaidi ya Sh50 milioni.
Mchimbaji mzoefu, Sophita Malembeka alisema
mashamba mengi yanayopakana na Mto na Mlima Mgongo yana dhahabu, hivyo
kuomba waruhusiwe kuchimba pia kuupasua mlima.
Wachimbaji wengi walisema kwa siku zinapatikana
gramu kati ya 100 na 200 za dhahabu ambazo katika eneo hilo zinauzwa
hadi Sh60,000 kwa gramu.
Mchimbaji mwingine, David Selea alisema kwa
wastani kama wakiwa na maji ya kutosha katika eneo la mita tano wamekuwa
wakipata kati ya gramu tatu hadi tano kwa siku.
Mnunuzi wa madini, Charles Malongo kutoka Bariadi,
Simiyu alisema kwa siku hununua hadi gramu 100 na dhahabu ya eneo hilo
ni bora kwa asilimia 99.
NA MWANACHI
0 comments:
Post a Comment