HESLB WAFUNGUKA,WASEMA :VYUO VILIVYOKAMILISHA TARATIBU VIMESHAPELEKEWA FEDHA ZA MIKOPO
Mkurugenzi wa Habari,Elimu na Mawasiliano wa HELSB, Cosmas Mwaisobwa
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya
Juu (HESLB), imesema kwa kiwango kikubwa vyuo ambavyo vimetimiza vigezo,
utaratibu wa kupata mikopo kwa ajili ya wanafunzi wake kwa mwaka
2014/15 umekamilika.
Kulikuwapo na madai kwamba fedha hizo zitachelewa kwa kuwa serikali imepeleka fedha nyingi katika Bunge Maalum la Katiba.
QAkizumngumzia
madai hayo, Mkurugenzi wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa HELSB, Cosmas
Mwaisobwa, alisema kuwa vyuo ambavyo havijapelekewa fedha muda wao wa
kupelekewa bado.
“Suala
la kusema fedha zimeelekezwa katika Bunge la Katiba mimi siwezi
kulizungumzia, kwa kuwa mimi siyo mwanasiasa,” alisema Mwaisobwa na
kuongeza:
“Kwa
vyuo ambavyo bado havijapata mkopo ni kutokana na kutofikia tarehe ya
vyuo husika kupata mikopo. Kwa hiyo wasije wakatamani kwa kuona wenzao
ambao tarehe yao ilifika mapema ya kupata mkopo, wasubiri na wao zamu
yao itafika. Mfano, Chuo cha Tumaini wameshapata, lakini Chuo cha Ruaha
bado.”
Mwenyekiti
wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO),
Musa Mdede, alipoulizwa kuhusu suala hilo, alisema vyuo ambavyo tarehe
ya kupata mkopo wameshapelekewa hundi kwa ajili ya kusainiwa ili
wapatiwe fedha.
“Nina
taarifa za chuo cha SAUT cha Mwanza, UDSM, IFM, DIT naTumaini kwamba
wameshapelekewa hundi na vingine ambavyo vipo Dar es Salaam. Na mara
nyingi kuchelewa au kuwahi kufika kwa fedha za mkopo chuoni kunategemea
zaidi ni lini chuo husika kinafunguliwa,” alisema Mdede.
0 comments:
Post a Comment