TAARIFA MPYA KUHUSU ILE NDEGE YA MALAYSIA ILIYOPOTEA KUTOLEWA
Taarifa
ya picha kamili za Satelite kuhusu ndege ya Malaysia iliyopotea MH370
zitatolewa kesho kwa mujibu wa maafisa wa nchi hiyo.
Kaimu
waziri wa usafirishaji wa Malaysia Hishammuddin Hussein ametoa taarifa
kuhusu kutolewa data za ndege hiyo wakati akiwa anatembelea kampuni
iliyopo katika uwanja wa ndege wa Kuala Lumpur.
Familia
na ndugu wa abiria waliokuwemo ndani ya ndege hiyo iliyopotea mwezi
Machi mwaka huu ikiwa imebeba watu 239 katika eneo Kusini mwa Asia
wamekuwa wakidai data za ajali hiyo kuwekwa hadharani.
Hatma ya waliokuwemo ndani ya ndege hiyo bado imebaki kuwa moja ya kitendawili kikubwa kuwahi kutokea katika nyakati za sasa.
Kampuni
ya Inmarsat, ambayo Satelite yake ilikuwa ikiwasiliana na ndege hiyo
iliyopotea katika dakika za mwisho imesema kuwa haikupewa kibali na
mamlaka za Malaysia kuachia taarifa hizo hadharani.
Lakini sasa kampuni hiyo na serikali ya Malasysia wanasema wanajaribu kufanya taarifa hizo zitolewe hadharani.
0 comments:
Post a Comment