Wednesday, 7 May 2014

Hii kali Shinyanga!! MWANAMKE AHUKUMIWA JELA MIEZI 12 KWA KUSINGIZIA MTOTO KWA MWANAMME MWINGINE ILI APATE PESA YA MATUMIZI,JAMAA KALEA MTOTO ASIYE WAKE KWA MIAKA MITATU BILA KUJUA

PICHA TOKA MAKTABA
Mahakama ya mwanzo ya Old Shinyanga mkoani Shinyanga imemhukumu mwanamke mmoja Pendo  Joachim (33) mkazi wa kata ya Old Shinyanga kutumikia kifungo cha nje ya gereza kwa muda wa miezi 12 na kulipa faini ya shilingi milioni moja baada ya kupatikana na kosa la kusingizia mtoto kwa mwanaume mwingine ili apate pesa za matumizi.
Akitoa hukumu hiyo jana,hakimu wa mahakama ya mwanzo ya Old Shinyanga Christina Chovenye alisema mahakama hiyo baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na mashahidi imemhukumu Pendo Joachim kutumikia kifungo cha nje cha miezi 12 na faini ya shilingi milioni moja ili liwe fundisho kwa watu wengine.
Chovenye alisema mahakama hiyo imemtia hatiani Pendo Joachim chini ya kifungu cha sheria cha 304 sura ya 16 kilichofanyiwa marekebisho mwaka 2002 kwa kosa la udanganyifu ambapo Deus Njile amekuwa akimuhudumia mtoto huyo kwa muda wa miaka 3 akijua kuwa ni mtoto wake
Kwa upande wake mshitakiwa Pendo Joachim alipotakiwaa kujitetea aliomba kupunguziwa adhabu kwa kuwa ana watoto wawili wanaomtegemea na kwamba anasumbuliwa na ugonjwa wa shinikizo la damu.
Deus Njile alisema kuwa alibaini kuwa mtoto sio wake baada ya kuona kadi mbili za kliniki zenye majina tofauti ya baba ndipo alipoamua kwenda kwenye uongozi wa kijiji ili kupata suluhu ndipo Pendo Joachim alikiri kuwa mtoto huyo ni wa mwanaume mwingine.
Katika Kesi hiyo yenye namba 24 ya mwaka 2014 ili funguliwa tarehe 19/3/2014,imeelezwa kuwa Pendo Joachim alikuwa akisingizia kuwa mtoto wake anayetumia jina la Edward Deus ni wa bwana Deus Njile na kusababisha Deus Njile kumhudumia mtoto huyo kama wa kwake kwa muda wa miaka mitatu.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA