Maajabu ya Dunia!!! WANAKIJIJI WANYESHEWA MVUA YA SAMAKI HUKO SRI LANKA
Samaki waliotoka mtoni kutokana na upepo mkali |
Samaki hawa ambao walikuwa katika hali nzuri ya kuweza kulika wanaaminika kuwa walibebwa kutoka kwa mto kwa upepo mkali.
Hili si tukio la kwanza la aina hii
kuwahi kutokea Sri Lanka- mwaka wa 2012, kulitokea kisa cha mvua ya
viumbe vya baharini vijulikanavyo kama 'Kamba' ambavyo huliwa na wanakijiji
hao wa wilaya ya Chilaw walisema kuwa walisikia kitu kizito kikianguka
na wakapata samaki wengi wenye uzani wa kilo hamsini .
Wanasayansi wamesema kuwa mvua ya Samaki
hutokea wakati ambapo upepo mkali unazinga juu ya maji ya kina kifupi
na hivyo kusababisha mzunguko wa maji unaovuta karibu kila kitu kilicho
ndani ya maji ikiwa ni pamoja na samaki na hata Vyura.
Viumbe hawa wa majini wanaweza
wakasafirishwa kwa masafa marefu kwa kushikiliwa na mawingu hata baada
ya ule mzunguko wa maji kuisha.
Wanakijiji wanasema kuwa mvua hiyo ya
Samaki ilinyesha Jumatatu huku viumbe wale wakianguka kwenye mashamba,
barabara na paa za kijiji hicho.
Baadhi ya samaki hao wenye urefu wa kati
ya sentimita tano na nane, walikuwa bado wako hai na walitiwa kwenye
ndoo za maji na wanakijiji waliowatumia kama kitoweo badaye.
Hii ni mara ya tatu kwa tukio kama hili kufanyika Sri Lanka, ingawa katika eneo tofauti.
Kando na ile mvua ya ‘Prawn’ya mwaka wa
2012 kusini mwa Sri Lanka, mvua ya kimondo (meteors) nyekundu na manjano
ilinyesha mwaka huo huo,tukio ambalo bado linachunguzwa na wanasayansi
wa Marekani na Uingereza.
CHANZO- BBC
0 comments:
Post a Comment