HII NDIYO KAULI YA COSTA KUHUSU KUJIUNGA NA CHELSEA MAJIRA YA JOTO ISOME HAPA
MSHAMBULIAJI
wa Atletico Madrid, Diego Costa, ameitandika Chelsea bila huruma na
kuisaidia klabu yake kufuzu fainali licha ya kuwepo kwa tetesi kuwa
atajiunga na Chelsea majira ya kiangazi mwaka huu.
Costa
alifunga bao la penati na katika ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Chelsea
na kumfanya Diego Simeone akutane na Carlo Ancelotti katika mchezo wa
fainali mjini Lisbon nchini Ureno mwezi ujao.
Mtandao huu kupita mtandao rafiki wa Goal.com unafahamu kuwa Chelsea wametenga kitita cha pauni milioni 35 kukamilisha usajili wa nyota huyo mwenye miaka 25.
Costa amekiri kuwa kwasasa hajaamua maisha yake ya baadaye.
“Kucheza Chelsea baadaye? Tutaona, najua kuna ofa kwa ajili yangu, najisikia vizuri kuwepo Atletico” ameuambia mtandao wa Sky Italy.
Adrian Lopez na Arda Turan pia walifunga, lakini Chelsea walikuwa wa kwanza kufumania nyavu za Atletico kupitia Fernando Torres.
Costa
ameuelezea mchezo wa leo kuwa ni “wa maajabu na historia” na amemsifu
kocha wake Diego Simeone kuifanya Atletico kuwa na makali zaidi msimu
huu.
“Ni kitu cha ajabu na kihistoria. Tumejituma kwa nguvu zote kufika fainali hii”. Costa amezungumza na Canal Plus.
“Mpira
haukuishia kwenye penati tu, lakini ulimalizika vizuri. Nadhani timu
inafanya vitu sahihi, lakini Diego Simeone amefanikiwa kufanya maamuzi
sahihi kila wakati
NA GAOL.COM
0 comments:
Post a Comment