Huyu ndie amemtukana Rais na kusema aache Bangi kilichofuata ni hiki
Sio jambo
la kawaida mtu kujiamini na kumtukana Rais wa nchi na taarifa hiyo
kuripotiwa kwenye vyombo vya habari lakini kwa Samuel Onkwami imekua
rahisi kwake ila imemgharimu maana sasa hivi yuko kwenye sehemu
atakayoshughulikiwa.
Ni
mwakilishi wa Wadi ya Kiogoro Kaunti ya kisii huko Kenya na sasa
amefikishwa Mahakamani kwa tuhuma za kudai kwamba Rais Uhuru Kenyatta
anavuta Bangi ambapo ishu ilianzia pale alipokaririwa Kanisani
akihutubia na kusema ‘walio karibu na Rais Uhuru Kenyatta sharti
wamshauri aache kuvuta Bangi’’
Kiongozi
wa mashtaka ameiambia mahakama ya kisii kwamba mwakilishi huyo wa wadi
alitoa matamshi hayo katika kijiji cha karera na sheria inayo mshtaki
mtuhumiwa inasema ni hatia kwa yeyote kutoa matamshi kama hayo kuhusu
mtumishi wa umma .
Samuel
ambae ni baba ya watoto watano anataaluma ya Teknolojia ya maabara
kutoka chuo kikuu cha Teknolojia Mombasa na amewahi kuhudumu katika
ofisi za hazina ya ustawishaji eneo Bunge kabla ya kuingia kwenye siasa
mwaka wa 2007 na baadae kuchaguliwa mwaka uliopita kuwa mwakilishi wa
Wadi.
Mawakili
wa mshukiwa ambao ni Gideon Nyambati na Isaiah Mosota wameiomba mahakama
hiyo kumuachia huru mshukiwa kwa dhamana na kuomba upande wa mashtaka
kuwapa ushahidi na malalamishi dhidi ya mteja wao ili kujiandaa vyema
kwa ajili ya kutoa utetezi wao.
Mshtakiwa ameachiliwa kwa dhamana ya shilingi 20,000 pesa za Kenya na Kesi hiyo itatajwa May 14 na kusikilizwa June 3 2014.
0 comments:
Post a Comment