Mzungu anayeizunguka dunia akitembea kwa miguu, awasili nchini
Raia wa
Urusi, Sergey Chikachev, akizungumza na mwandishi wa gazeti la hili
mkoani Kilimanjaro, Daniel Mjema (hayupo pichani) mjini Moshi jana,
kuhusu safari yake ya kutembelea mataifa mbalimbali kwa miguu, tayari
amekwisha tembelea mataifa 80 na hivi sasa yupo nchini. Picha na Dionis
Nyato
Moshi. Raia
wa Urusi, Sergey Chikachev anayezunguka mataifa mbalimbali duniani kwa
miguu, juzi amewasili nchini akitokea Kenya na anatazamiwa kuzunguka
mikoa mbalimbali kwa siku 30.Akizungumza
na gazeti hili mjini Moshi jana, Chikachev ambaye ameshazunguka mataifa
80, alisema akiwa nchini, atakwenda vijijini kujifunza utamaduni na
maisha ya makabila mbalimbali.“Kwa
siku chache tangu niwasili hapa (Moshi) nimebaini Watanzania ni watu
wenye hazina kubwa ya ukaribu… naamini nitajifunza mengi
yatakayonisaidia kuandika kitabu changu,”alisema.
Chikachev
alisema atakitumia kitabu chake hicho, kupeleka ujumbe wa amani kwa
mataifa hayo na kuhamasisha urafiki kati ya makabila ya mataifa
mbalimbali atakayoyatembelea duniani.
Kwa
mujibu wa Chikachev, alianza kutembelea mataifa hayo kwa miguu tangu
mwaka 2004 na ameshazunguka Ulaya, Asia, Australia, Marekani na sasa
bara la Afrika ambapo kwa sasa yupo nchini Tanzania.
Chikachev
alisema baada ya kumaliza safari yake nchini, anatarajia kwenda Uganda,
Rwanda, Burundi, Namibia, Botswana, Congo, Nigeria na baadaye Cameroon
na atahitimisha ziara zake hizo mwaka 2017.
Hata
hivyo alisema safari yake hiyo imekuwa ikikutana na changamoto nyingi na
wakati mwingine amekuwa akipata lifti kutoka kwa madereva wa malori
lakini hilo limekuwa likitokea mara chache.
Raia huyo
wa Urusi alisema kwa baadhi ya mataifa, amekuwa akipatiwa ufadhili wa
usafiri wa ndege au majini katika maeneo ambayo hawezi kutembea kwa
miguu kutoka taifa moja kwenda lingine.
0 comments:
Post a Comment