MAJANGA GEITA!! KIJANA AJINYONGA HADI KUFA KWENYE CHOO CHA MAMA MKWE WAKE,ALITAKA MAPENZI KINYUME NA MAUMBILE AKAKIMBIWA NA MKEWE
Kijana mmoja aliyefahamika kwa
jina la Daudi James(33) mkazi wa mtaa wa Shilabela mjini Geita mkoani
Geita amekutwa amekufa kwa kujinyonga chooni kwa mama mkwe wake kwa
kutumia kitenge.
Walioshuhudia tukio hilo
wamesema limetokea usiku wa kuamkia leo ambapo Daud James amekutwa
amejinyonga chooni kwa mama mkwe wake eneo la General Tyre.
Akizungumzia tukio hilo mama
mkwe wa marehemu Lucia Magulu(32) amesema marehemu alimuoa binti yake
Dorothea Jacksoni(18) mwaka mmoja uliopita huku akiwa na ujauzito wa
mwanamme mwingine na baada ya kujifungua wameendelea kuishi na mtoto wao
ambaye ni Hellena mwenye umri wa miezi kumi.
"Jana jioni alipofika hapa
nyumbani alikaa hadi walipomaliza kula chakula cha jioni na alipoambiwa
arudi nyumbani kwake Shilabela alikataa na kutaka aende na mke wake
",anaeleza mama mkwe.
"Baadae mke wake alipomkatalia
kwenda marehemu alimuomba kitenge mke wake kwa maelezo ya kuwa anaenda
kulala kwa rafiki zake na ndipo alipopewa,cha kushangaza na kusikitisha
leo asubuhi tumemkuta kajinyonga kwa kitenge hicho chooni",ameongeza
mama mkwe.
Kamanda wa polisi mkoani Geita Joseph Konyo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa
uchunguzi bado unaendelea ili kubaini sababu gani zilipelekea kifo chake.
Hata hivyo kamanda Konyo
ameitaka jamii kuacha mambo ya kujichukulia maamuzi ya kujiua bila
sababu za msingi huku akiwataka waandishi wa habari nao kuelimisha jamii
iachane na tabia za kujinyonga kila mara wanapokuwa wamezozana na wake
zao.
Hili ni tukio la pili kutokea
ndani ya siku tatu ambapo juzi mkazi wa tambukareli mjini Geita
alijinyonga na kijining’iniza kwenye mti wa mpera baada ya kuhitlafiana
na mke wake.
Na Valence Robert wa Malunde1 Blog -Geita
0 comments:
Post a Comment