MAN CITY WAKARIBIA UBINGWA ..WAICHAPA ASTON VILLA 4-0
Mtu wa heshima: Edin Dzeko akiunguruma baada ya kufunga bao lake la kwanza leo Etihad dhidi ya Aston Villa.
KWA
asilimia kubwa mnuso wa ubingwa wanukia Etihad baada ya Manchester City
kuibuka na ushindi mtamu wa mabao 4-0 dhidi ya Aston Villa katika
mchezo wa ligi kuu soka nchini England.
Dakika 45 za kipindi cha kwanza zilimalizika kwa milango ya timu zote kuwa migumu.
Baada
ya kuingia katika vyumba vya kuvalia nguo, Manuel Pellegrini
aliwakumbusha vijana wake kuwa wamebakiwa na kazi ndogo kuchukua taji.
Man City waliporudi kipindi cha pili walikuja na kasi nzuri na katika dakika ya 64 na 72, Edin Dzeko alifunga mabao mawili.
Wakati Aston Villa wakitafuta njia ya kusawazisha, katika dakika ya 89, Stefan Jovetic aliifungia bao la tatu Man City.
Dakika
ya 93, mwafrika mwenye kiwango cha juu zaidi, Yaya Toure alihitimisha
karamu ya mabao na kuwafanya City wakaribie kuutwaa ubingwa wa pili
ndani ya misimu mitatu.
City
wameishusha Liverpool kileleni kwa kufikisha pointi 83, huku Liverpool
wakibakia nafasi ya pili kwa poini 81. Timu zote zimecheza mechi 37.
Sare
ya mabao 3-3 waliyopata Liverpool jumatatu ya wiki hii dhidi ya Crystal
Palace imewafanya wawe katika wakati mgumu wa kufuta ukame wa miaka 24
bila kombe, na sasa wanawaombea dua mbaya Man City wafungwe mechi ya
mwisho siku ya jumapili dhidi ya West Ham kwenye uwanja wa Etihad.
Dzeko akiungana na wachezaji wa Man City kushangilia bao lake la pili.
Kikosi cha Man City leo: Hart, Zabaleta, Kompany, Demichelis, Kolarov, Javi Garcia, Toure, Milner, Silva, Nasri, Dzeko.
Wachezaji wa akiba: Richards, Lescott, Negredo, Clichy, Fernandinho, Pantilimon, Jovetic.
Kikosi cha Aston Villa: Guzan, Lowton, Vlaar, Baker, Clark, Bertrand, El Ahmadi, Westwood, Delph, Weimann, Bowery.
Wachezaji wa akiba: Bacuna, Steer, Sylla, Tonev, Holt, Robinson, Grealish.
Mwamuzi: Michael Oliver
Kikosi cha Aston Villa: Guzan, Lowton, Vlaar, Baker, Clark, Bertrand, El Ahmadi, Westwood, Delph, Weimann, Bowery.
Wachezaji wa akiba: Bacuna, Steer, Sylla, Tonev, Holt, Robinson, Grealish.
Mwamuzi: Michael Oliver
Vitu vya hatari vya nahodha wa Man City Kompany
Shuti kali: Mshambuliaji wa Villa Andreas Weimann (kulia) akiachia shuti kali lililompita beki wa City Pablo Zabaleta
Hataki kutazama: Manuel Pellegrini yupo katika asilimia kubwa ya kutwaa taji la ligi kuu.
Aleksandar Kolarov akipiga mpira wa adhabu ndogo
Zuia kule bwana wewe!: Kocha wa Aston Villa, Paul Lambert akitoa maelekezo kwa wachezaji wake
Almanusura apige vitu: Samir Nasri alikosa nafasi nzuri ya kuifungia bao Manchester City
Vita: Mfungaji mkali, Dzeko (kushoto) akichuana na beki wa Aston Villa, Karim El Ahmadi
Ishara nazo zipo: Shabiki mmoja wa Man City akionesha bango la kumkejeli Steven Gerrard
Maombi kwa sana: Joe Hart akiomba baada ya timu yake kukaribia kutwaa ubingwa wa ligi kuu.
Katika mchezo mwingine, maajabu ya soka yameendelea kutokea kwa Sunderland baada ya usiku wa leo kushinda mabao 2-0 dhidi ya West Brom.
BAADA YA MECHI ZA LEO MSIMAMO WA EPL KWA TIMU 10 ZA JUU HUU HAPA
Katika mchezo mwingine, maajabu ya soka yameendelea kutokea kwa Sunderland baada ya usiku wa leo kushinda mabao 2-0 dhidi ya West Brom.
BAADA YA MECHI ZA LEO MSIMAMO WA EPL KWA TIMU 10 ZA JUU HUU HAPA
ENGLISH BARCLAYS PREMIER LEAGUE | LOGS
Pos | Team | P | W | D | L | GF | GA | GD | Pts |
1 | Manchester City | 37 | 26 | 5 | 6 | 100 | 37 | 63 | 83 |
2 | Liverpool | 37 | 25 | 6 | 6 | 99 | 49 | 50 | 81 |
3 | Chelsea | 37 | 24 | 7 | 6 | 69 | 26 | 43 | 79 |
4 | Arsenal | 37 | 23 | 7 | 7 | 66 | 41 | 25 | 76 |
5 | Everton | 37 | 20 | 9 | 8 | 59 | 39 | 20 | 69 |
6 | Tottenham Hotspur | 37 | 20 | 6 | 11 | 52 | 51 | 1 | 66 |
7 | Manchester United | 37 | 19 | 6 | 12 | 63 | 42 | 21 | 63 |
8 | Southampton | 37 | 15 | 10 | 12 | 53 | 45 | 8 | 55 |
9 | Newcastle United | 37 | 15 | 4 | 18 | 42 | 57 | -15 | 49 |
10 | Stoke City | 37 | 12 | 11 | 14 | 43 | 51 | -8 | 47 |
0 comments:
Post a Comment