MASCHERANO AFUNGUKA""UFALME WA BARCELONA HISPANIA NA ULAYA UMEKWISHA,"""
KIUNGO
wa Barcelona, Javier Mascherano amekiri kuwa ufalme wa klabu hiyo
katika soka la Hispania na Ulaya kwa ujumla umefika kikomo.
Wakatalunya
walishindwa kutetea ubingwa wao wa La Liga baada ya kushindwa kuwafunga
Atletico Madrid kwenye uwanja wa Camp Nou jana usiku na kumpa nafasi
Diego Simeone kunyakua `ndoo`.
Atletico Madrid licha ya kuwabania Barca kutetea taji lao, pia waliwatoa katika hatua ya robo fainali ya UEFA.
Mambo
yalikuwa mabaya zaidi kwa Barca baada ya kufungwa na Real Madrid katika
fainali ya Copa del Rey na sare ya jana imewafanya wamalize msimu bila
kombe.
Mascherano
anaamini kufanya vibaya msimu huu kunadhihirisha kuwa ufalme wa
Barcelona umefikia kikomo na yanatakiwa mabadiliko makubwa, lakini
alikaa kimya kuhusu hatima yake ya baadaye klabuni hapo.
“Kuzungumzia hatima ya Mascherano ni jambo dogo sana, kinachotakiwa ni kuizungumzia Barcelona. Ufalme umekwisha.” Aliambia Barca TV.
“klabu itafanya maamuzi na mabadiliko, lakini lazima tukubali kuwa msimu huu haukuwa mzuri”.
Kocha
Tata Martino amethibitisha kuondoka Barcelona majira ya kiangazi mwaka
huu, huku Luis Enrique akitarajiwa kurithi mikoba yake.
0 comments:
Post a Comment