MGONJWA ASHINIKIZA KUHARAKISHIWA KIFO CHAKE ILI ACHANGIE VIUNGO VYAKE KWA WENGINE
Sherri Muzher (kushoto) na Dk Jack Kervorkian. |
Mwanamke
aliyefikia hatua za mwisho kabisa za uhai kutokana na ugonjwa
anapambana kuhitimisha maisha yake ili aweze kuchangia viungo vyake
kuwezesha wengine waishi.
Sherri
Muzher, mwenye miaka 43, kutoka Detroit, Michigan, alikuwa na miaka 27
tu pale alipogundulika na ugonjwa wa kukacha kwa tishu wakati wa majira
ya joto baada ya mwaka wake wa kwanza katika shule ya sheria.
Hali
hiyo ya kutoponyeka, ambayo husababisha mfumo wa kinga kushambulia
mfumo wa fahamu mwilini, umeshuhudia mwili wake ukidhoofika kwa kasi,
ukimwacha akiwa hawezi kutembea na kuongea kwa shida.
"Ni
heri nisaidie kuwapa uhai wengine wakati viungo vyangu vingali vinaweza
kutumika,"alisema. "Ni ukweli wangu. Ninazidi kudhoofika. Misuli dhaifu
katika kuongea kwangu, kila kitu. Hii kwa haraka inafikisha ukweli
mahali pake."
Kuhusiana
na hali yake, aliongeza: "Ni hasara kubwa - hasara kwa kuongezeka MS.
Ni mchakato wa kusikitisha, sababu unapoteza uhuru wako kwa kasi."
Mtaalamu
wa weledi wa kitabibu alisema wakati kesi ya Muzher ikivutia mno,
inatatizwa na ukweli kwamba anaishi mjini Michigan, ambayo bado
inawindwa na kesi ya Dk Jack Kervorkian.
Daktari
huyo, ambaye alipachikwa jina 'Dokta Kifo', alikuwa mwanaharakati wa
kifo cha huruma ambaye alidai kuwa alisaidia vifo vingi vinavyofikia
130.
Mwaka
1999, alikamatwa na kujaribiwa kwa mchango wake katika kesi ya kifo cha
hiari na akatumikia miaka minane ya hukumu ya kifungo cha miaka 10 hadi
25.
"Inafikiri hiyo itawezekana [sheria hiyo inaweza kubadilika mjini
Michigan], lakini ni kitu fulani ambacho mjini Michigan pekee kinaweza
kuzusha utata mno hasa kwa kuzingatia historia ya Dk Kevorkian," alisema
Lance Gable, profesa wa sheria katika Chuo Kikuu cha Wayne State.
"Ushawishi wake unaonekana kukatisha mno tamaa. Anataka hatamu zote
za hatima yake na pia kusaidia watu wengine, na nafikiri hiyo ni habari
inayovutia mno kusimulia."
Kujiua kwa msaada wa daktari inaruhusiwa kisheria huko Oregon, Washington, Vermont na Montana pekee.
Mweledi wa tiba Dk Michael Stellini alisema kwamba kesi hiyo itawasilishwa kwa matatizo.
"Kama tunasubiri kwa muda mrefu, hatoweza kuchangia," alisema. Kama
tutafanya mapema mno, hatokuwa mwishoni, na hiyo inaibua mambo yote
yanayohusu masuala ya weledi."
Aliongeza kwamba sheria inaweza pia kuibua maswali mengi yahusuyo weledi katika siku za usoni.
Lakini wakati Muzher akisema mapafu yake hayawezi tena kufaa,
anaamini kwamba kwa kuruhusiwa kufa pale atakapochagua kutamwezesha
kugawa kwa figo, maini, moyo na viungo vingine kwa wote wanaohitaji.
"Ni heri nibaki mwenye umuhimu na msaada, kuliko kutupiliwa mbali na
kutokuwa na uwezo wa kusaidia," alisema. "Kitakachonipa faraja ni
kufahamu nimeacha urithi wa kuwapatia uhai wengine."
0 comments:
Post a Comment