NAPE AFUNGUKA: ANENA MAZITO..:KUHUSU CCM KUWABEMBELEZA UKAWA...!
.
Kamati
Kuu ya Chama cha Mapinduzi chini ya Mwenyekiti wake Rais DK JAKAYA
KIKWETE ilikutana Dodoma May 5 2014 ili kujadili na kuzungumzia masuala
mbalimbali ikiwemo mchakato wa Bunge la Katiba ambalo limesitishwa mpaka
mwezi wa nane.
Akitoa
mapendekezo ya Kamati Kuu, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Nape
Nnauye amesema licha ya kutoa mapendekezo yatakayofanikisha upatikanaji
wa katiba mpya, chama hicho kimepinga vitendo vya baadhi ya wabunge
kupinga waziwazi kwenye majukwaa juu ya kuendelea kwa bunge
Maalum. Namkariri akisema ‘kamati kuu pia inasikitishwa na juhudi za
makusudi za baadhi ya watu au vikundi vya watu kuamua kuendeleza
upotoshaji kuhusu
mchakato
mzima wa mabadiliko ya katiba, wameamua kupotosha kwa kwenda
barabarani, kufanya mikutano au kuzungumza na Waandishi wa habari
kupotosha baadhi ya mambo’Kwenye sentensi nyingine Nape amesema chama
chake hakipo tayari kuwabembeleza wajumbe waliosusia kuhudhuria vikao
kwa kusisitiza ‘hatuna mpango wa kuzungumza nao na tunampango wa
kushughulika nao mtaani wanakokwenda, sio sisi na wala hatuna mpango wa
kuishawishi Serikali wala viongozi wa kitaifa kuwabembeleza kuwarudisha
bungeni, mimi nadhani waendelee kukaa barabarani’
na MATUKIO NA VIJANA blg
0 comments:
Post a Comment