Cesc Fabregas ametoswa na Van Gaal.
Imechapishwa Mei 26, 2014, saa 12:55 jioni
KOCHA wa Manchester United, Louis van
Gaal amewafuta Cesc Fabregas na Toni Kroos katika mipango yake ya
usajili majira ya kiangazi mwaka huu.
Mholanzi
huyo sasa ameanza kuhusishwa na usajili wa kiungo nyota wa Bayern
Munich , Bastian
Schweinsteiger na kinachosubiriwa kwasasa ni neno la Pep Guardiola
ambaye yuko tayari kusikiliza ofa ya paundi milioni 10 ili kumuachia
nyota huyo mwenye miaka 29.
Schweinsteiger, aliyetajwa kuwindwa na United tangu enzi za Moyes bado yupo katika rada za kocha mpya Van Gaal.
Toni Kroos naye amepotezewa baada ya kuleta nyodo.
Louis van Gaal ametaja wachezaji wengi anaowahitaji atakapojiunga na Man United
Kwenye mawindo: Bastian Schweinsteiger anaweza kuuzwa kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 10.
Fabregas anaweza kuondoka Barcelona majira ya kiangazi mwaka huu baada ya kushindwa kung`ara
Van Gaal pia anamtupia macho beki wa Uholanzi Daryl Janmaat (kushoto)
NA BK MTATA
0 comments:
Post a Comment