TAARIFA ZA JESHI LA POLISI KUHUSU VURUGU ZILIZOTOKEA DODOMA
Kutoka
Dodoma Mei 05 majira ya saa saba mchana kulitokea vurugu zilizoanzishwa
na wabeba mizigo wa Mji mdogo wa Kibaigwa ambapo taarifa inasema zilikua
ni vurugu zilizosababisha magari kadhaa kuvunjwa vioo.
Miongoni
mwa magari yaliovunjwa vioo ni pamoja na la Mbunge wa Tanga Omary
Nundu,gari la Polisi na basi linalofanya safari zake kati ya Dar na
Mwanza la Shabaha mbali na kuvunjwa kwa magari hayo pia maduka yaliporwa
na hata barabara kuu ya Dodoma-Morogoro ilifungwa.
Kamanda
wa Polisi mkoa wa Dodoma amesema David Misime amesema Mpaka sasa jeshi
la polisi linawashikiliwa watu 34 ambao ni wakazi wa kibaigwa kata ya
kibaigwa wilaya ya kongwa kwa makosa ya kufanya fujo na kuharibu mali.
Sehemu
nyingine ya taarifa hiyo inasema vijana zaidi ya 300 wakishirikiana na
wabeba mizigo wa Kibaigwa walifanya maandamano yasiyo na kibali na
kung’oa bango la halmashauri ya kongwa lililokua na tangazo la kukataza
wafanyabiashara kuingiza mazao sokoni bila kulipa ushuru.
Baada ya
bango hilo vijana hao waliamua kufunga barabara kuu ya Dodoma Morogoro
kwa mawe na kuchoma matairi baadae walivamia maduka na kupora vinywaji
na kuvunja majokofu.
Chanzo
cha vurugu hizo ni wabeba mizigo wa soko la mazao Kibaigwa kupinga
kitendo cha Halmashauri ya Kongwa kuweka tangazo la kutoza ushuru wa
mazao sokoni hapo wakidai kwamba inawakosesha kufanya kazi zao kwani
wateja wao wanashindwa kuingiza mazao sokoni.
na matukio na vijana blg
0 comments:
Post a Comment