Monday, 26 May 2014

Waziri wa Usalama wa taifa wa Somalia ajiuzulu

 

Waziri wa Usalama wa Taifa wa Somalia amejiuzulu. Abdikarim Hussein Guled amejiuzulu baada ya kujiri shambulio la kigaidi karibu na bunge la Somalia mjini Mogadishu hapo jana. 
Taarifa zinasema kuwa, baada ya shambulio hilo lililopelekea watu 10 kuuawa, waziri huyo wa usalama wa Somalia alishinikizwa na wabungen ajiuzulu.
Wakati huo huo Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limelaani shambulio hilo lililofanywa na wanamgambo wa al Shabab kwenye jengo la bunge la Somalia. 
Wajumbe wa Baraza la Usalama wamesema kuwa wanasikitishwa na shambulio hilo dhidi ya bunge taasisi ambayo inawakilisha wananchi wa Somalia, na ambako ni mahala wanapotumaini kupata usalama, amani na maendeleo kwa njia halali.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA