Tumewanasa viongozi wa ‘Mbwa Mwitu’
Kamanda wa Polisi kanda hiyo, Kamishna Suleiman Kova
Dar es Salaam. Jeshi la Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam
limewakamata watu sita wanaodaiwa ni viongozi wa kundi la ‘Mbwa Mwitu’
linalojihusisha na vitendo vya uvamizi na uporaji wa mali za watu kwenye
nyumba na maduka jijini humo.
Kamanda wa olisi kanda hiyo, Kamishna Suleiman Kova alisema kutokana na
kukamatwa kwa viongozi hao na kupatikana kwa taarifa za makundi hayo
jeshi lake litafanya msako wa nyumba kwa nyumba, mtaa kwa mtaa hadi
wahusika wote wakamatwe.
Hawa viongozi tunao, tumeshawahoji na wamekiri ni kweli wamekuwa
wakijihusisha na vitendo hivyo kwa kutumia makundi yao,” alisema Kova na
kuongeza: “Sisi tunaanza kuwasaka hao vijana kwa sababu tumeshapata
taarifa za kutosha kutoka kwa wenzao…tunafahamu wapi pa kuwapata.”
Aliwataja waliokamatwa kuwa ni Athuman Said (20), Joseph Ponela na
Clement Peter (25) wakazi wa Kigogo, Roma Vitus (37), Mwanshishe
Adam(37) na Daniel Peter (25)wakazi wa Temeke.
Taarifa hiyo imekuja siku moja baada ya kusambaa kwa taarifa za kundi
hilo la vijana zaidi ya 300 kuvamia mitaa mbalimbali ya jiji hilo,
kupora mali na kujeruhi watu.
Kamishna Kova alisema kuwa jeshi lake lilifanikiwa kuwakamata viongozi
hao baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema akisisitiza kwamba
hatua inayofuata ni kuwasaka vijana wanaowatuma kufanya uhalifu huo.
“Hii itakuwa operesheni endelevu tunayoianza mwezi huu hadi mwezi Julai
mpaka tuhakikishe tumewakamata wahalifu hawa na tatizo hili
limetokomea,”alisema Kova kwa msisitizo.
Alisema jeshi lake limejipanga kukabiliana na wahalifu hao na kuwa
wananchi waache kuwa na hofu kutokana na taarifa za uvumi zinazosambazwa
kwenye mitandao kuhusu uhalifu unaofanywa na vijama hao.
“Ningependa kuwatoa hofu wananchi kuhusiana na uvumi unaoendelea kwenye
mitandao…tunaomba wananchi wawe watulivu waendelee na shughuli zao kama
kawaida. Jeshi langu limejipanga vizuri kuwadhibiti hao vijana. Hao
vijana hawana uwezo wa kutushinda sisi” alisema Kova
Kamanda huyo aliweka wazi kuwa askari wa kutosha wa doria wameshapangwa
maeneo ambayo yametajwa kuwa na mlipuko wa makundi hayo.Maeneo hayo ni
pamoja na Kigogo, Manzese, Magomeni na Mbagala.
Mwananchi
0 comments:
Post a Comment