England yaanza vibaya kombe la dunia.....Yachapwa 2-1 na Italia,, Uruguay yakalia kuti la Moto....Yachapwa 3-1 na Costa Rica, Suarez akalia benchi mwanzo mwisho
Straika wa Italia, Mario Balotelli (kushoto) akiifungia timu yake bao la ushindi dhidi ya England usiku huu.
Timu ya Taifa ya England imeanza vibaya kombe la dunia baada ya kukubali kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya timu ya Taifa ya Italia maarufu kwa jina la Azzuri mjini Manaus katika mchezo wa kundi D.
Italia walikuwa wa kwanza kuandika bao la kuongoza katika dakika ya 35 kupitia kwa Claudio
Marchisio, lakini katika dakika ya 37, Daniel Sturridge aliisawazishia
England bao hilo akiunganisha krosi nzuri iliyochongwa na Wayne Rooney
kutoka wingi ya kushoto.
`Supa` Mario Balotelli ndiye aliwaua England baada ya kuandika bao la pili kwa njia ya kichwa katika dakika ya 50.
Kikosi cha England kilichoanza: Hart, Johnson, Cahill, Jaglielka, Baines, Gerrard, Henderson, Sterling, Rooney, Welbeck and Sturridge
Kikosi
cha Italia kilichoanza: Sirigu, Chiellini, Paletta, Barzagli, Darmian,
De Rossi, Pirlo, Veratti, Candreva, Marchisio and Balotelli.
KIKOSI cha Uruguay kimelala kwa bao 3-1
dhidi ya Costa Rica katika mechi ya kundi D kwenye Fainali za Kombe la
Dunia 2014 zinazoendelea nchini Brazil.
Katika mechi hiyo, mshambuliaji mahiri wa Uruguay na Liverpool Luis Suarez alianzia benchi na kumalizia mechi benchi yaani hakucheza kabisa licha ya kuwepo kwenye orodha ya wachezaji wa akiba, na hii inatokana na kushindwa kuimarika ipasavyo kutoka kwenye majeruhi ya goti alilofanyiwa upasuaji.
Katika mechi hiyo, mshambuliaji mahiri wa Uruguay na Liverpool Luis Suarez alianzia benchi na kumalizia mechi benchi yaani hakucheza kabisa licha ya kuwepo kwenye orodha ya wachezaji wa akiba, na hii inatokana na kushindwa kuimarika ipasavyo kutoka kwenye majeruhi ya goti alilofanyiwa upasuaji.
Wafungaji wa Costa Rica waliopeleka maumivu
Uruguay ni Joel Campbell, Oscar Duarte na Marcos Urena. Uruguay
walipata bao lao kwa mkwaju wa penalti kupitia kwa Edinson Cavani.
0 comments:
Post a Comment