Wednesday 15 April 2015

MWANAMUZIKI PERCY SLEDGE AFARIKI KWA UGONJWA KWA SARATANI

Percy Sledge enzi za uhai wake.
MTUNZI wa wimbo maarufu wa 'When a Man Loves a Woman', amefariki jana nyumbani kwake Baton Rouge, Jimbo la Lousiana, Marekani, akiwa na umri wa miaka 73  baada ya kusumbuliwa muda mrefu kwa ugonjwa wa saratani.
Percy Sledge ambaye alikuwa mahiri katika miondoko ya R&B, alivuma sana mwaka 1966 ambapo wimbo wake huo uliposhika namba moja katika anga la muziki nchini Marekani na kimataifa.  Ulipotolewa kwa mara ya pili nchini Uingereza mwaka 1987, bado ulishika nafasi ya pili.
Kama hiyo haitoshi, mwanamuziki Michael Bolton alipokuja kuutoa mwaka 1991, wimbo huo ulishika namba moja.  Hadi leo, bado ni moja ya nyimbo maarufu katika duru za filamu huko Hollywood, Marekani, na umetumika katika filamu zaidi ya 20.
Nyimbo nyingine ambazo Sledge alizitoa na kupata umaarufu mkubwa ni  "Warm and Tender Love" na  "Take Time to Know Her"  ambazo, hata hivyo, hazifikii rekodi yake hiyo iliyotingisha anga la burudani ya muziki duniani.
Mwanamuziki huyo aliendelea kufanya maonyesho hadi kiasi cha mwaka mmoja uliopita ambapo kesho (Alhamisi) wimbo wake wa "When a Man Loves a Woman" utakuwa umefikisha miaka 49 tangu utungwe.
-GPL

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA