Utabiri MPYA wa Nabii: Mwanamuziki mkubwa wa Bongo Fleva atafia Jukwaani kabla ya kumalizika kwa mwaka huu wa 2014
Nabii anayetikisa kwa maono ya vitu mbalimbali Hosea Chamungu 'Mzee wa maono' ameibuka na jambo zito baada ya kufunga kwa siku tatu mfululizo huku akifanya maombi nyikani......
Akiongea na mwanahabari wetu mapema wiki hii, nabii Chamungu alisema kuwa amekuwa na desturi ya kufunga siku tatu kila wiki ili kupata maono ya mambo mbalimbali yanayojiri hapa duniani.....
Chamungu ambaye kabla ya unabii amewahi kuwa mwanachama wa Freemasons amesema alichofunuliwa hivi majuzi ni kwamba bado vifo vitaendelea kuwaandama wasanii mbalimbali na kabla ya kumalizika kwa mwaka huu wa 2014 kuna msanii mkubwa wa mziki wa Bongo Fleva atafia jukwaani.....
"Atafariki kwa ajili ya pesa na itakuwa jukwaani, yawezekana akawa anagombea pesa au anatunzwa pesa jukwaani ndipo umauti utakapomkuta," alisema Chamungu huku akisisitiza kuwa hayo ni maono na si hadithi.
Chamungu alifafanua kuwa vifo vinavyohusisha pesa hutokana na shetani ambao ni jamii ya Lucifer na Illuminati ambapo pia hujulikana kama Freemasons....
"Kifo chake kitavuta hisia za watu wengi wakiwemo wakawaida na maarufu kama ilivyotokea kwa marehemu Kanumba lakini hatazikwa na watu wengi kama alivyozikwa Kanumba," alisema
0 comments:
Post a Comment