Thursday 19 June 2014

HII KALI***Mtoto wa miaka tisa anayemfanyia ukatili mama yake, amshikia kisu akitaka kumuua

bobbi2
Wewe unadhani ukatili wa kijinsia ni kwa wazazi au walezi tu kwenda kwa watoto? Hapana hata kwa baadhi ya wazazi pia inatokea kwa kufanyiwa ukatili na watoto wao ila hushindwa kujitokeza hadharani kusema mbele ya jamii kwa aibu au kufanya hivyo mara chache.Hii imemtokea mwanamke huyu aitwaye Bobbi kutoka Southampton , Uingereza ambapo anasimulia jinsi alivyofanyiwa ukatili na mtoto wake mwenye umri wa miaka tisa akitaka kumchoma kisu na wakati mwingine kumvizia akitaka kumuua.

bobbi
Mtoto huyo aitwaye JJ mara kadhaa amekuwa akifanya mashambulizi ya vurugu kwa mama yake kwa kumpiga, kumrushia vitu kichwani na wakati mwingine kumvuta nywele ambapo katika tukio jingine alijaribu kumchoma kisu akitaka kumuua.
bobbi3
Hali hiyo ilimlazimu Bobbi kuondoa vitu vyote vyenye ncha kali karibu na nyumbani ili kuepusha hatari ambapo hata kwa baba yake wa kambo imekuwa ngumu kwake kuishi pamoja na mtoto huyo kwani ni vita kali.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA