ROSE MUHANDO KUZINDUA FACEBOOK AGOSTI 3/2014
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari kwenye viwanja vya Karimjee leo wakati alipokua akitangaza Uzinduzi mkubwa wa Albam ya Shikilia Pindo maarufu ka FACEBOOK ya mwimbaji wa muziki wa injili anayevuma Rose Muhando utakaofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee Agosti 3 /2014 jijini Dar es salaam, ambapo amesema baadhi ya mapato yatakwenda kuviwezesha mitaji zaidi ya vituo 10 vya watoto yatima jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akifafanua zaidi kwa waandishi kuhusu uzinduzi huo unaoarajiwa kuwa mkubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki kwa waimbaji wa muziki wa injili.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akiwaeleza zaidi waandishi na kusema taarifa zaidi zitaendelea kutolewa ili kuwajulisha mashabiki wa muziki wa injili juu ya uzinduzi huo.
0 comments:
Post a Comment