Thursday, 5 June 2014

ZIMESALIA SIKU 7 KABLA YA KUANZA KOMBE LA DUNIA

bra_ba63e.jpg
Je wajua kwamba...
Ili kuhakikisha usalama wa watu wengi watakaokwenda Brazil kutazama mechi, ndege zisizo na rubani zitatumika kufanya doria. Ndege hizo - drones- aina ya PackBot 510 hutumiwa na jeshi la Marekani. Zinaweza kuongozwa kutoka mbali na huweza kung'amua vitu vya hatari au kwenda sehemu za hatari.

Mbali na ndege hizo pamoja na maroboti ya Kimarekani kulinda usalama, miwani zenye camera zinazoweza kutambua sura za watu pamoja na vifaa vyenye teknolojia ya kisasa vitatumika kulinda usalama wa raia na watalii. Wanajeshi wa Brazil ndio watakuwa wakilinda usalama katika miji ambayo mechi zitachezwa.
Waamuzi 25 wa FIFA watachezesha mechi za Kombe la Dunia. Waamuzi hao wanatoka katika mabara yote sita, na wote watachezesha angalau mechi isiyopungua moja. Waamuzi hao na wasaidizi wao watakuwa wakifuatiliwa kwa karibu na kupewa kila msaada wanaohitaji na FIFA ili waweze kuchezesha kwa haki.
Afrika kupitia CAF inawakilishwa na Noumandiez Doué (Ivory Coast), Bakary Gassama (Gambia) na Djamel Haimoudi (Algeria). Mwamuzi aliyechezesha fainali ya mwaka 2010 Howard Webb kutoka England ni miongoni mwa waamuzi walioteuliwa kutoka UEFA

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA