ANGALIA PICHA MAPOKEZI YA DIAMOND PLATNUMZ AKITOKEA MAREKANI KATIKA TUZO ZA BET
09:20 |
No Comments |
Tarehe 10/7/2014 ni siku ambayo Star wa muziki wa Bongo fleva nchini Tanzania Diamond Platnumz, ambaye anachafua anga la muziki kwa sasa kwa utunzi na uimbaji wake alitua katika Uwanja wa Ndege Mwal. Jurius Nyerere, mnamo mishare ya saa nne na nusu za usiku akitokea nchini Marekani ambapo alikua huko kushiriki katika Tuzo kubwa Dunia BET awards, ambazo hufanyika kila mwaka, Diamond alikua katika kategori ya Best African Act ambayo ilichukuliwa na Davido kutoka Nigeria.

Watanzania wenye moyo wa Upendo na Kizalendo walijitokeza katika viwanja vya ndege kumpokea Msanii huyo, wakiwa na mabango makubwa kabisa yenye maneno ya kuashiria ushujaa aliouonyesha Diamond katika muziki na kuipeperusha vyema Bendera ya Tanzania katika muziki, Uwanja wa ndege wa Mwl. Julius Nyerere, uligubikwa na Kelele za Furaha na Sauti zilisikika zikiimba wimbo wa Mdogomdogo ikiwa ni mapenzi ya dhati kabisa kwa Diamond kwa kutuwakilisha vema na kurejea salama, hakika kazi ya muziki wetu kwa sasa inaonekana.
Diamond baada ya kufika aliwashukuru wote waliofika kumpokea na kusema kuwa safari yake ilikua nzuri na amejifunza vitu vingi sana pia amekutana na watu wengi na tutaraji mengine mengi na mazuri katika muziki wetu, na kwa upande mwingine alitoa shukran za dhati kabisa kwa watanzania kuipokea vema video yake mpya ya mdogomdogo, imekua ikifanya vizuri sana na hata youtube imekuwa na views wengi kwa muda mchache
Related Posts:
CHEKI PICHA SHOO YA DIAMOND DAR LIVE ILIVONOGA Mwanamuziki Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' akipozi katika picha na mashabiki baada ya shoo ya nguvu Dar Live. Diamond akiwa na tuzo pamoj… Read More
RAY C ASEMA HAYA BAADA YA KUANDIKWA KWENYE GAZETI KUWA AMEREJEA KWENYE UTEJA ‘DAKTARI:JK MUOKOE RAY C’ NDIO KICHWA CHA HABARI CHA MAGAZETI ILIYOMTOA MACHOREHEMA CHALAMILA AKA RAY C ILIYOANDIKWA NA GAZETI LIITWALO ‘AMANI’… Read More
VANESSA MDEE ASHINDA TUZO ZA AFRIMA NCHINI NIGERIA! Msanii wa bongo fleva Tanzania, Vanessa Mdee akiwa ameshikilia tuzo hiyo mara baada ya kukabithiwa!Vanessa Mdee ashinda tuzo ya msanii bora w… Read More
HUYU MTOTO NI SHIDAAH !! CHEKI LULU AKIFANYA YAKE BUKOBA NI ZAIDI YA BATA Mwigizaji wa filamu,mrembo na mwenye mvuto wa kufanya wengi wapagawe, Elizabeth Michael aka Lulu ambae kwasasa yupo Mjini Bukoba kwa … Read More
SHINDANO LA MISS TANZANIA LAFUNGIWA MIAKA MIWILI KUTOKANA NA KUKIUKA UTARATIBU Tangu atangazwe aliyekuwa Miss Tanzania 2014 Sitti Mtemvu mengi yameongelewa kuhusiana na tetesi za udanganyifu wa umri na vitu vingine … Read More
0 comments:
Post a Comment