Friday, 11 July 2014

HIZI NDIZO SABABU ZA DIAMOND KUTUMIA WAZUNGU KWENYE VIDEO YAKE MPYA ""MDOGO MDOGO""



Kumekuwa na maoni tofauti kuhusiana na video ya ‘Mdogo mdogo’ ya Diamond Platnumz iliyotoka Jumatatu ya wiki hii. Wapo ambao wamefurahishwa na story iliyoko kwenye video hiyo na wengine ambao hawajaiunga mkono moja kwa moja kutokana na kila mmoja kuwa na sababu tofauti hali ambayo imeleta mabishano mengi katika comments za youtube na kwingine.

Lakini inawezekana wengi ama wote hatujui maana halisi ya story iliyoko kwenye video hiyo na sababu za Diamond na timu yake kuamua kuifanya hivyo ilivyo.
Diamond amefunguka jinsi story ya video hiyo ilivyozaliwa na script kuandikwa:

“Ujumbe ulikuwa kwamba mapenzi yanakuwa hayachagui rangi wala kabila na kuutoa ubaguzi kama mtoto flani labda muhindi hawezi kuolewa na mswahili au mzungu, mswahili hawezi kumuoa muhindi au mzungu au mchina no no no…haya ni mapenzi na wote mkiridhiana yaendane yakubalike tu. So hiyo ilikuwa message, lakini pia nikaamua kuifanya kisehemu mbili tofauti tofauti ili pia kutokupoteza culture halisi ya kitanzania. Ndio maana utaona kuna character moja ndo naigiza mimi kijijini kabisa kama Tarzan yaani kama mtu wa kijijini kabisa halafu yule ndio mtoto wa mfalme ambaye ndio ananipenda mimi hapa.” Amesema Diamond kupitia 255 ya XXL ya Clouds FM.


Diamond pia amemtaja director maarufu wa bongo movie marehemu Adam Kuambiana kuwa ndiye mtu aliyeleta wazo la script iliyotumika kwenye video hiyo na baadae kuongezewa chachandu na mpenzi wake Wema Sepetu.


“Script wakati inaanza kwanza nilikuwa sasa mimi nataka kufanya kitu flani lakini nilikuwa sijui nakianzaje…so nakumbuka that time Adam Kuambiana alikuwa anadirect movie ya kina baby nilikua naenda kambini nakutana naye, na baby aliniambia ni mzuri sana, nikamfata nikamwambia bana na wimbo wangu nataka uniandikie story …akasema basi itakua vizuri nikifika studio na nuiisikilize….akaskiliza ngoma akawa ananipa namna story inavyotakiwa kuanza kwenda. So naweza kusema mwanzoni wakati story inavyoanza picha hata ya kuipata story ni Kuambiana ndo alinipaso baada ya hapo mi nikaenda nikakaa nayo nyumbani mi na baby tukakaa baby nikamwambia Kuambiana katoa wazo kama hili unaona tulifanyeje, so tukakaa unajua baby nae master katika maswala ya movie movie, so akakaa akawa anaiandika hapa iwe hivi aah isiwe hivi hapa iwe hivi, baada ya kumaliza kuiandika akaichora katika lugha ngeni tukaituma kwa director akaitazama na akaipitisha.”


Platnumz ameongeza kuwa video hiyo imemgharimu dola elfu 32 pamoja na gharama za kusafiri yeye na timu yake hadi Afrika Kusini.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA