KESI YA MBASHA YASOMWA LEO,JUA KILICHOJIRI
Mara baada ya nusu saa kupita Wakili wa mshitakiwa alituma muakilishi wake kuwakilisha barua za dharula ambazo zilionesha kuwa yupo safarini mkoani Arusha na kuomba kesi hiyo kuahirishwa.Emanuel Mbasha ana kabiliwa na kesi mbili za ubakaji ambapo inadaiwa alitenda makosa hayo maeneo ya Tabata katika nyakati mbili tofauti,Mbasha alisindikizwa mahakamani na ndugu zake huku Mkewe Flora Mbasha kutoonekana Mahakamani na badala yake alionekana mdogo wake Flora ambaye ni shemeji yake Emanuel Mbasha.
Kesi hii imehairishwa mpaka July 23 mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment