MAMA AMCHOMA KISU NA KUMUUA MWALIMU MBELE YA WANAFUNZI WAKE
Mwanamke mmoja ameripotiwa kumchoma kisu na kumuua mwalimu wa kike wa shule ya msingi mbele ya wanafunzi wake katika mji wa Albi ulio kusini mwa Ufaransa.
Muendesha Mashtaka wa Albi, Claude Derens ameiambia AFP kuwa tukio hilo limetokea jana (July 4) majira ya asubuhi kwa saa za Ufaransa na kwamba uchunguzi unafanyika ili kubaini sababu zilizopelekea mwanamke huyo kufanya tukio hilo la kikatili.
“Mama huyo alionekana akiwa na kisu na akamchoma mwalimu wa kike mwenye umri wa miaka 34 mbele ya wanafunzi wake, sababu itafahamika baada ya uchunguzi kukamilika.” Claude Derens aliiambia AFP.
Aliongeza kuwa baada ya tukio hilo, rais wa Ufaransa Francois Hollande alimtuma waziri wa elimu, Benoit Hamon haraka katika shule hiyo ili kuhakikisha anachukua hatua kama mwakilishi wa serikali.
-NA Dunia kiganjani
0 comments:
Post a Comment