Mambo 26 yasiyojulikana na vijana wengi na ambayo hupelekea umaskini
1. Usijilinganishe Maisha yako na watu wengine, huwezi jua wao wanatumia njia gani kufanikiwa
2. Usiwe na mawazo hasi kwenye vitu usivyo na uwezo navyo, ila wekeza nguvu zako katika kila ulifanyanlo sasa na utafanikiwa.
3. Usifanye kazi kwa kujitesa na nje ya uwezo wako, fanya kazi kwa kadri ya uwezo wako
4. Usijiumize sana kufikiria ya baadae, jaribu kuwa makini na wakati uliopo kwani ndio utakueleza baadae yako itakuaje
5. Usimalize nguvu zako katika umbea, chuki na majungu
6. Ota ndoto za mafanikio ukiwa macho, hakikisha unajitahidi kutimiza malengo yako kwa kufanya mikakati yako kuwa na mashiko
7. Kumbuka una kila kitu cha kukufanya ufanikiwe, mfano afya, akili, na fursa mbele yako
8. Kamwe usijikite katika yaliyopita au kumkumbusha mtu yoyote mambo yaliyopita kwani yanaweza kuiharibu furaha ya sasa
9. Maisha ni mafupi sana hivyo usipoteze muda kumchukia mtu yeyote yule
10. Sahau na kukubaliana na makosa yako ya zamani ili yasije kukuharibia mipango ya sasa
11. Hakuna atakaekuja kukupa furaha katika Maisha ako zaidi yako wewe mwenyewe
12. Kumbuka Maisha ni chuo na upo kwa ajili ya kujifunza hivyo tengeneza CV yako vyema kwani kila ujifunzacho kina maana katika Maisha yako ya sasa na ya baadae.
13. JItahidi kufurahi kila mara na kila siku kwani ni dawa tosha ya kukupunguzia maumivu ya Maisha
14. Usitake kushinda kila mabishano/majadiliano , jaribu kukubalina au kukataa
15. Wasilina na famila yako mara kwa mara
16. Kila siku fanya kitu chenye kuwafurahisha wakuzungukao na Mungu wako
17. Uwe mtu wa kusamehe na kusahau
18. Pata muda wa kuzungumza na watu wenye umri wa miaka 70 na miaka chini ya 6 kuna mengi ya kujifunza
19. JItahidi angalau watu 3 uwafurahishe kwa siku
20. Vitu ambavyo watu wanaviwaza kuhusu wewe havikuhusu hivyo kuwa mpole
21. Kazi yako haitakuuguza ukiwa unaumwa, hivyo jitahidi kuwa na mahusiano mazuri na familia na marafiki
22. Umfanye MUNGU awe wa kwanza katika kila kitu unachokifikiria au kukifanya na utafanikiwa kwani MUNGU ni muweza wa vyote
23. Fanya vitu vyenye uhalisia na uwe tayari kwa kila matokeo
24. Pamoja na shida na majaribu uliyonayo jitahidi kutoifanya dunia itambue hilo
25. Kila siku kabla ya kulala mshukuru MUNGU kwa siku nzuri na ukiamka asubuhi hakikisha unamshukuru MUNGU kwa kukuamsha salama
26. Kama unamfahamu MUNGU kila siku utaishi kwa furaha sana na kumbuka ishi kwa furaha kama kila siku ndio siku yako ya mwisho kuishi hapa duniani
0 comments:
Post a Comment