MARTIN KADINDA AFUNGUKA::KUMBE ALITAMANI WEMA AWE WAKE::SOMA HAPA
MWANAMITINDO maarufu Bongo, Martin Kadinda amesema kabla hajawa kiongozi wake, awali aliwahi kumtamani kimapenzi mcheza filamu Wema Sepetu, lakini alighairi baada ya kugundua ni mwanamke wa kudekadeka.
Kadinda alitoa kauli hiyo hivi karibuni wakati akipiga stori na paparazzi wetu kuhusu masuala mbalimbali yanayomhusu msichana huyo ambaye ana uhusiano wa kimapenzi na mkali wa Bongo Fleva, Diamond Platinumz.
Kuhusu maisha wanayoishi nyota hao wawili wapenzi, Kadinda alisema kwa jinsi wanavyoishi ni kama watu wanaoigiza, akitolea mfano wa kipindi walichorudiana wakiwa nchini China, ambako wenyewe walisema wanaigiza filamu wakati ndiyo kwanza walikuwa wanarejesha penzi lao lililovunjika mara ya kwanza.
0 comments:
Post a Comment