Wednesday 6 August 2014

BARCELONA KUANDAA PAUNDI 10 MIL KUMNASA THOMAS VERMAELEN

Barcelona inajiandaa kutoa kiasi cha fedha paundi 10m kwa ajili ya kumsajili mlinzi wa Arsenal Thomas Vermaelen.Mlinzi huyo wa kimataifa wa Ubelgiji anatakiwa pia na Manchester United na Arsenal inaweza kupendezwa zaidi kumuuza mlinzi huyo nje ya England lakini itafikiria kumuuza kwa fedha ya juu. Arsenal inadai kwamba Vermaelen, 28, ana thamani ya paundi 12m.
United wamepanga kukutana kwa ajili hiyo baadaye wiki hii.Vita: Barcelona wako tayari kulipa paundi 10m kwa ajili ya kuharibu mipango ya Manchester United kwa Thomas Vermaelen
Kipindi kipya: Vijana wa Luis Enrique wako busy katika soko la wachezaji kipindi hiki cha usajili
Vermaelen ni nahodha wa sasa wa Arsenal, lakini alikuwa na wakati mgumu dhidi ya Laurent Koscielny na Per Mertesacker msimu uliopita.
Alikuwa kimya kipindi hiki,lakini anaweza kujiunga kati ya Barca au United. 
Wakati huo huo, Louis van Gaal amemsainisha mlinda mlango wa FK Vojvodina Vanja Milinkovic, 17.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA