RAIS OUATTARA ALIINGIA MADARAKANI KWA KUTUMIA NGUVU AKISAIDIWA NA UFARANSA
Rais wa
Zamani wa Ivory Coast President Laurent Gbagbo (Katikati) akiwa na
mwanasheria wake Emmanuel Altit (Kulia)t for the start of the trial at
the International Criminal Court in The Hague, Netherlands, January 28,
2016
Na Emmanuel Richard Makundi
Mawakili
wa utetezi wa rais wa zamani wa Ivory Coast, Laurent Gbagbo, wanamtuhumu
rais wa sasa, Alassane Ouattara kwa kuchukua madaraka kwa nguvu
akisaidiwa na taifa la magharibi lililowahi kuitawala nchi hiyo,
Ufaransa.
Katika
maelezo yao ya awali kwenye mahakama ya ICC ikiwa ni siku ya tatu toka
kuanza kwa kesi dhidi ya kiongozi huyo, ambapo wakili wake, Emmanuel
Altit ameileza mahakama namna ambavyo Ufaransa ilimsaidia Ouattara
kuchukua madaraka kwa nguvu.
Wakili
Altit, ameongeza kuwa, rais Ouattara na wafuasi wake, walitaka kuchukua
madaraka kwa nguvu ikiwa ni pamoja na kugombea mji wa Abidjan, ilikuwa
ni wazi kabisa kuwa mpango wake ulipangwa kwa kusaidiwa na Ufaransa.
Rais wa
zamani wa Ivory Coast, Laurent Gbagbo akiwa kwenye mahakama ya ICC mjini
The Haguerimes contre l'humanité, au premier jour de son procès devant
la CPI, jeudi 28 janvier 2016.
Gbagbo na
mtuhumiwa mwingine, Charles Ble Goude, kiongozi wa kundi la vijana
lililokuwa linamuunga mkono, wamekana mashtaka ya uhalifu dhidi ya
binadamu baada ya watu elfu 3 kuuawa wakati wa vurugu za mara baada ya
uchaguzi mkuu wa 2010.
Kesi hii
ya aina yake ambayo ni ya kwanza kushuhudia rais wa zamani akisimama
kizimbani, inatarajiwa kudumu kwa zaidi ya miaka mitatu.
Gbagbo
alijitangaza kuwa mshindi wa uchaguzi wa mwaka 2010, lakini mataifa
yenye nguvu duniani ikiwemo Marekani na Ufaransa pamoja na umoja wa
Mataifa walimuunga mkono Ouattara aliyeshinda kwa idadi ndogo ya kura.
Mawakili
wa Gbagbo wamewaambia majaji wa mahakama ya ICC, kuwamteja wao
ametengenezewa kesi, kesi ambayo wahusika wake ni taifa la Ufaransa,
ambalo lilihakikisha Ouattara anaingia madarakani kwa nguvu.
0 comments:
Post a Comment