LAANA YA MAMA YAKE YAMTISHA WEMA SEPETU

.Akizungumza na Mpekuzi, Wema alisema kuwa ndio maana kipindi ambacho mama yake hakutaka kuolewa na mchumba wake Nasibu Abdul 'Diamond' hakupenda kutumia nguvu ama uwezo wake wa kifedha kumpuuza mzazi wake kwani anaamini angemuumiza na kumfanya amtamkie maneno mabaya...
"Natambua fika kuwa Mungu ametuagiza kuwaheshimu wazazi wetu kwani hawa ni miungu wadogo, wakitamka neno lolote baya baada ya kuwaudhi huwa linaumbika na kuwa shida kwa mhusika, ndio maana wakati anaweka mikingamo ya mimi kuolewa na Diamond sikulazimisha bali niliendelea kumsihi akubali." Alisema Wema.

Penzi la Wema na Diamond linazidi kupamba moto hasa baada ya hivi karibuni kuvishana pete nyingine ya uchumba baada ya mama Wema kubariki penzi lao
0 comments:
Post a Comment