CHEKI HAPA YALIYOJIRI ENGLAND LEO MANCHESTER UNITED IKIAMBULIA MVUA YA MAGOLI NA MATOKEO MENGINE:
22:27 |
Man United ambao walishinda mechi iliyopita ya ligi dhidi ya QPR kwa ushindi wa magoli 4-0, leo hii wameonja kipigo kizito kutoka kwa Leicester, baada ya kukubali kufungwa 5-3.
Man United ndio waliokuwa wa kwanza kuliona lango la Leicester kupitia Robin van Persie, kabla ya dakika baadae Angel di Maria kuongeza la pili.
Dakika moja baada ya United kufunga goli la pili, Leicester wakafungw goli la
Kwanza kupitia Ulloa na mpaka mapumziko matokeo yalikuwa 2-1.
Kipindi cha pili Ander Hererra akaifungia Man United goli la 3, lakini dakika chache baadae Leicester wakapata penati na kufunga goli la pili, huku United wakiwa bado na hasira za kulalamikia maamuzi ya refa, Estaban Cambiasso akafunga goli la kusawazisha.
Mchezaji aliyeng’ara kwenye mchezo Jamie Vard akaifungia City goli la 4, kabla ya dakika baadae Nugent kufunga goli la tano kwa mkwaju wa penati.
Mpaka refa anapuliza kipenga cha mwisho Leicester City 5-3 Man United.
Katika mechi nyingine goli la Frank Lampard dakika ya 85 liliifanya Manchester City itoshane nguvu na timu ya Chelsea kwa bao moja kwa moja kufuatia goli la Andre schurie uwanja wa Etihad.
Totenham imechapwa bao moja na West Bromich Albion huku Everton ikibugizwa goli 3 kwa mbili na Crystal palace
Related Posts:
PICHA: MANCHESTER UNITED ,MANCHESTER CITY HAKUNA MBABE MANCHESTER UNITED (4-2-3-1): De Gea 6; Valencia 6.5 (Darmian 5.5), Jones 6.5, Smalling 7, Rojo 6.5; Schweinsteiger 7(Fellaini 6.5), Schneiderlin 6; … Read More
TAZAMA MATOKEO YA MECHI ZA UEFA JANA … Read More
LIVERPOOL YAITWANGA CHELSEA 3-1, SASA MOURINHO ASOGEA MLANGO WA KUTOKEA Kocha wa Liverpool akipongezana na beki Sakho Coutinho akipiga shuti kupachika bao la pili mbele ya nahodha Terry Chelsea ikiwa nyumbani &n… Read More
KOCHA WA LIVERPOOL HANA KIKOSI RASMI LAKINI ANAJIAMINI Kocha Jurgen Klopp ameonyesha kuwa uwezo mkubwa wa kujiamini akiwa na Liverpool inayoonekana kama haina kitu. Maana kwa mechi tano mfululizo,… Read More
STOKE CITY YAZIDI KUZAMISHA JAHAZI LA CHELSEA LIGI KUU Mdudu wa vipigo ameendelea kuiandama Chelsea baada ya kufungwa tena leo katika Ligi Kuu England baada ya kuchapwa kwa bao 1-0 dhidi ya Stoke City.… Read More