Friday, 12 September 2014

MWANAUME APATA HISIA ZA UJAUZITO


Harry Ashby ni mwanaume wa kwanza nchini Birmingham kupata ruhusa ya kupumzika nyumbani baada ya kusumbuliwa na homa mithili ya mwanamke mja mzito.Amekuwa akipatwa na homa za vipindi hasa nyakati za asubuhi baada ya mchumba wake aitwae Charlotte kuwa mjamzito, mtandao wa Itv news umeeleza.Habari zinasema mwanaume huyo mwenye miaka 29 anayefanya kazi ya ulinzi ,amesema
ameongezeka uzito na tumbo limekua mithili ya aliye mjamzito na kudai kuwa anasumbuliwa na maumivu ya mgongo na cha ajabu amekuwa na hamu ya baadhi ya vyakula
Harry ameripotiwa kuwa na dalili za kuwa mja mzito miezi miwili baada ya kubaini kuwa mchumba wake ni mjamzito.
Harry amekuwa akipatiwa dawa na inasemekana anaweza kudai mafao wakati akiwa katika mapumziko hayo.
CHANZO BBC

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA