SIR ALEX FERGUSON AONGOZA MKUTANO WA MWAKA WA MAKOCHA,
Tabasamu: Sir Alex Ferguson akizungumza na Carlo Ancelotti na Arsene Wenger katika mkutano wa makocha mjini Nyon
MKUTANO wa mwaka wa makocha wa kiwango cha juu umeanza jana jumatano na kumalizika leo, makao makuu ya UEFA, mjini Nyon, Uswizi.
Kocha wa zamani wa Manchester United, Sir Alex Ferguson alikuwa mwenyekiti wa mkutano huo akiwa kama balozi wa makocha wa UEFA , wakati naye Rais Michele Platini alikuwepo.
Wakizungumzia mchezo mzuri: Rais wa UEFA Michele Platini akizungumza na Ancelotti na Ferguson leo alhamisi.
Picha ya pamoja ya makocha katika makao makuu ya UEFA leo nchini Uswizi.
Mjadiliano: Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho akiwa amekaa na kocha wa zamani wa Stamford Bridge, Carlo Ancelotti
Mkali wa maneno: Mourinho akizungumza na waandishi wa habari nje ya makao makuu ya UEFA leo.
Hata hivyo, kocha wa mashetani wekundu, Manchester United, Louis van Gaal - ambaye ni mshindi wa Bundesliga, La Liga na Eredivisie - hakuwepo katika mkutano huo kwasababu timu yake haishiriki michuano ya UEFA mwaka huu.
Hakuwepo: Louis van Gaal hakuhudhuria mkutano huo.
0 comments:
Post a Comment