Wednesday, 10 September 2014

TANZANIA YAONGOZA KWA KULALAMIKIWA ,MATUMIZI MABAYA INSTAGRAM DUNIANI


Mtandao wa Instagram unaohusisha uwekaji picha umeendelea kupata mashabiki wengi nchini Tanzania lakini wengi kati ya watumiaji hao wameisababisha kuwa kati ya nchi zinazoongoza kwa matumizi mabaya ya mtandao huo duniani kote.
 
Ripoti hiyo imetolewa na Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasialiano Tanzania (TCRA), Innocent Mungy katika mahojiano maalum aliyofanya na Ibrahim Issa wa 100.5 Times Fm.

“Tanzania ni moja kati ya nchi ambazo zimeongoza kwa watu kulalamika kwamba matumizi yetu hayaendani na makusudio. Na hii inatokana na pale watu ambao wanawafuata watu wa` Tanzania kuona vitu wanavyoweka vitu wanavyoweka, ugomvi, matusi, picha za ajabu…za ngono na nini. Sasa watu huwa wanalalamika.” Amesema Innocent Mungy.
 
“Wanapolalamika, ule mtandao huwa unaweka record kwamba watu wengi waliolalamika kwenye mtandao huu kuhusu picha za watumiaji ambao wako Tanzania labda ni 20 wakilinganisha na sehemu nyingine ambazo idadi inakuwa ndogo zaidi.” Ameongeza.
 
Amefafanua kuwa kwenye mitandao yote ya kijamii, wakati wa kujiunga mtumiaji hupewa maelezo ya kurasa kadhaa kuhusu namna ya kutumia mtandao huo ikiwa ni pamoja na makatazo lakini watumiaji wengi wa Tanzania huwa hawayafuatilii/huyapuuza.
 
Mwisho, Mungy ametoa wito kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii nchini kuitumia mitandao hiyo kwa maendeleo na sio vinginevyo.
 
“Mitandao hii ya kijamii kama mawasiliano ni maendeleo. Matumizi ya mitandao sio mabaya ila watumiaji ndio wanafanya vitu vibaya. Ningewataka watanzania ambao wanatumia mawasiliano haya vibaya waache. Tuitumie vizuri.
 
"Na wale watu ambao unawaona wewe hawaendani na matumizi ambayo yanapendeza, wafute kwenye mtandao wako. Wa-Unlike, wa-Unfriend au wa-delete kabisa ili usione hayo mambo yao ya kipuuzi wanayofanya.”
 
Credit: Ibrahim Issa (Times Fm)

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA