KILIMANJARO PREMIUM LAGER YAKUTANA NA WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI KUZUNGUMZIA KAMPENI YA “NANI MTANI JEMBE 2”
Story na Thade Expensive
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe akizungumza na baadhi ya wahariri wa vyombo habari jijini Dar es Salaam mchana wa leo,wakati wa semina ya kuzungumzia uzinduzi wa Kampeni ya Nani Mtani Jembe sehemu ya 2,utakaofanyika kesho tarehe 4 Oktoba 2014 katika viwanja vya Leaders Club,Kinondoni jijini Dar es salaam.
Afisa Uhusiano wa Kampuni ya Executive Solutions ambao ndio wanaoratibu Kampeni hiyo ya Nani Mtani Jembe 2,Ibrahim Kyaruzi akizungumza jambo kwenye mkutano huo.
baadhi ya wahariri wa vyombo habari jijini Dar es Salaam wakifatilia kwa makini semina hiyo.
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe akielezea namna Kampeni hiyo itakavyokuwa ikifanyika.
Sambamba na hilo mechi ya mtani jembe itakuwa siku ya tarehe 13 mwezi wa kumi na mbili na mwaka huu TBL wameboresha kwani kutakuwa na zawadi ya shilingi mil 100 ambako mashabiki watapata shilingi mil 80 na mshindi wa mechi atapata mil 20.
Vilevile safari hii kutakuwa na kipindi maalumu cha "mtani jembe chat" kitakachoruka kwa wiki mara moja pamoja na zawadi kwa watu watakao kuwa wanashiriki kila mara hao watapata zawadi ya shilingi 5000.