KUHUSU DIAMOND KUHOJIWA POLISI, NA KUSALIMISHA MAGWANDA YA JESHI, CHEKI HAPA
MSANII wa Muziki wa Kizazi kipya nchini,Naseeb Abdul maarufu kama Diamond Platnumz amehojiwa na Jeshi la Polisi baada ya kuonekana na mavazi halisi ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika Tamasha la Fiesta lililofanyika jijini Dar mwishoni mwa wiki.
Diamond amejikuta hapo siku moja tu baada ya Meneja wake Babu Tale kukamatwa jana kwa kuhojiwa na kulala mahabusu kuhusiana na matumizi hayo ya mavazi ya kijeshi katika onyesho la Fiesta.
Habari zinasema Diamond naye alijisalimisha mwenyewe polisi ambako baada ya mahojiano aliachiwa kwa dhamana. Magwanda aliyokuwa nayo aliyakabidi polisi wakati uchunguzi ukiendelea.
Habari zinasema Diamond naye alijisalimisha mwenyewe polisi ambako baada ya mahojiano aliachiwa kwa dhamana. Magwanda aliyokuwa nayo aliyakabidi polisi wakati uchunguzi ukiendelea.
- MICHUZI BLOG