KUTANA NA FAMILIA INAYOISHI NA MYAMA HATARI SIMBA
Kwenye nyumba tunazoishi mara nyingi tumekua tukifuga na kuishi na Paka au Mbwa kitu ambacho ni kawaida na ni nadra sana kukutana na mtu anaeishi na au kufuga viumbe ambavyo ni hatari kwa maisha ya binadamu mfano Nyoka.

Unaambiwa Simba huyu alihamia kwenye nyumba hiyo toka Melanie akiwa na umri wa miaka 14 huko Sherman Oaks,California Marekani ambapo mama yake Melanie ni mwigizaji Tippi Hedren na baba yake wa kambo kwa muda huo Noel Marshall. 

Kingine cha kufahamu ni kwamba hii familia ilikuwa inamlea Simba huyu nyumbani ambae alipewa jina la Neil kama wanyama wengine, mfano Mbwa au Paka. Picha za Melanie na mama yake wakiwa wanacheza na simba huyo ziliwekwa kwenye jarida la ‘Life Magazine‘ mwaka 1971 ambapo zilikua zinaonesha mtoto huyo kuwa na ukaribu mkubwa na Simba na hata kulala na kuogelea nae.
Mama Melanie aliyeigiza kwenye filamu ya ‘The Birds’ miaka 8 baada ya kupigwa kwa picha hizo alionekana pia kupenda kucheza na mnyama huyo pori.
Simba huyu alikuja kuishi na familia hiyo wakati mama Melanie na baba wakiwa wanatengeneza filamu Afrika ambapo kwenye matembezi yao waliona kuna nyumba yenye Simba ambao hawana makazi mazuri ndipo walipoamua kumchukua Simba huyo kutengeneza filamu inayohusiana na Simba.
Kweli baadae walitengeza filamu iliyoitwa ‘Roar’ ambapo ilitolewa kwenye miaka ya 80 ambapo kwenye mahojiano yaliyofanywa mwezi April mwaka 1982 na The Guardian, U.K ilitangazwa filamu hiyo ya Roar.
