IJUE BIMA NA FAIDA ZAKE
Ni mfumo wa kulipa kiasi cha pesa katika kampuni ya bima ili kujiinua au kujilinda na madhara ya tukio lolote baya litakalotokea katika kitu ulichokatia bima.
Kampuni ya bima inachukua jukumu la kurudisha hali iliyochafuka kuwa safi katika mazingira yoyote ya mtu aliyekata bima kwao.
Zipo bima za mfumo na aina tofauti tofauti hapa tutazifafanua kwa ufupi chache:
1.Bima ya dhima(Liability Insurance) bima hii humsaidia aliyekata kukwepa deni kwa mali aliyoharibu kwani yenyewe inalipia gharama hiyo.
Kwa mfano ikitokea mtu aliyekata bima hii akapata ajali ya kugongana na gari nyingine basi kampuni ya bima hubeba jukumu la kulipa mali iliyoharibiwa na aliyekata hii bima na haitahusika na kulipa gharama za mali ya aliyekata bima hii.
2.Bima ya maisha(Life Insurance) Hii uhusika zaidi na kuwalipa watu waliorodheshwa na mtu aliyekata bima kama wafaidika pindi anapoaga dunia.
3.Bima ya mali(Property Insurance) Hii inahusika zaidi na gharama ya kufidia Jengo na samani zote zitakazokuwa ndani ya jengo pindi inapopatwa na majanga kama ya moto, mafuriko au majanga mengine ya asili.
Hapa kwetu Tanzania siku hizi kuna kampuni nyingi sana za bima zimeanzishwa kwa hiyo siyo kitu kibaya kuandaa mazingira ya kulinda maisha ya watu wanaokuzunguka.
Hii ndio taarifa fupi juu ya bima asanteni.
0 comments:
Post a Comment